Wadau,
Nimekuwa nikifuatilia mijadala inayoendelea katika forum hii. Nataka kutoa changamoto kwa wadau wenzangu ili tujadili swali lifuatalo:
Je, ni mtanzania gani ana SIFA na VIGEZO vya kuiongoza Tanzania? Wachangiaji wanaweza kupendekeza majina MATATU.
Itakuwa vyema kama wachangiaji watatoa sababu zinazowafanya watoe mapendekezo hayo?
Nawasilisha hoja:
UPDATE:
Majina Matatu (makubwa) Yaliyopendekezwa:
- Jakaya Kikwete - CCM
- Willibrod Slaa - CHADEMA
- Ibrahim Lipumba - CUF
Uongozi ni kazi ngumu, ni kazi inahitaji muda na kujitoa kweli kweli katika kuhakikisha kwamba Taifa linafika kule ambako wote kwa pamoja tunaamini ni muhimu taifa lifike. Maeneo ambayo kwa pamoja kunamakubalino bila kujali ni nani anachanganua vizuri zaidi ni kama yafuatayo:-
1. Wote tunahitaji huduma bora za jamii-huduma hizi ni Afya, Elimu pamoja na miundombinu bora katika nchi yetu. Miundombinu hapa ni barabara, njia za reli n.k
2. Wote tunahitaji uchumi unatoa fursa kwa watanzania kuumilki. Tunataka uchumi ambao kukua kwake kunamnufaisha moja kwa moja mtanzania bila kujali kwamba yuko kwenye kundi gani la jamii ya watanzania. Uchumi unaotoa fursa sawia kwa kila mwenye kuthubutu kufanya kazi kwa akili na kwa kujituma. Kwa pamoja tunataka kuona uchumi ambukizi kutoka juu kwenda chini ( Economic multiplicity).
3. Wote kwa pamoja tunakubalina kwa namna fulani kwamba maliasili tulizonazo zinatosha kuiendesha inchi na kuwasaidia Watanzania kupata huduma muhimu ambazo wanataka. Misitu yetu, Milima yetu, Wanyama wetu , Bahari na maziwa na vyote tulivyonavyo kama malia ya asili vitumike kuleta neema kwa Watanzania.
Ili kufanya haya tunayo kubalina kwa pamoja kwa namna fulani kuwa kwa faida yetu sote tunahitaji kiongozi wa sifa zifuatazo:-
1. Kiongozi mwenye maono ya Tanzania ipi tunaitaka hapo baadaye. Kiongozi ambaye anaiangalia Tanzania kwa miaka mingi ijayo. Kiongozi huyu atoe dira ya Taifa letu lijalo na awe tayari kusimamia hilo
2. Kiongozi mwenye kuthubutu kufanya maamuzi magumu, haijalishi kwamba anaweza kukosana na wenzake lakini awe ni kiongozi mwenye kuthubutu kuamua njia ya kufuata na kupambana na hali yoyote ile kwa manufaa ya Taifa lake. Uongozi ni kujitoa mhanga kwa ajili ya Taifa kwa gharama yoyote
3. Kiongozi mwenye, wa kukemea, kuonya, kufundisha, kuelekeza na kuelimisha wengine wapi Taifa lipaswa kwenda kwa juhudi zake mwenyewe.
Kutokana na sifa hizi, ninashawishika, nijiaminisha na kujisaidikisha kwamba Dr. Willibroad Peter Slaa kwa juhudi na maarifa yake binafsi amethubutu kuzitafuta sifa hizi za kiongozi bora. Sifa hizi amezipata kwa kujibidisha kwake katika kujifunza kwa kusoma sana, kutafuta kwa njia ya kutafiti sana kila analotaka kusema na kulichangia, kujitoa kwa kuthubutu kusimama pekee yake katika kile anachoamini kwa kukemea, kuelimisha, kushawishi, kuonya n.k bila kuhofu kwamba atatengwa na wenzake kwa kufanya hivyo amelisaidia Taifa kuwa katika mwerekeo mpya kisiasa tulionao sasa. Sifa hizi hana Jakaya Mrisho Kikwete wala Ibrahimu Haruna Lipumba. Sifa hizi za Dr.Slaa hazifuati dini bali ni sifa za mtu binafsi kutokana na bidii ya kujitafutia maarifa na ufahamu lakini pia kuwa tayari kufa kwa kusema ukweli. Tanzania imeharibiwa kiutawala kupitia viongozi wa kisiasa tunahitaji kiongozi makini sasa ili kuiondoa nchi katika umaskini tuliomo na uzembe unao endelea katika utendaji wa maisha ya kila siku. Dr.Slaa anaweza kuwa sehemu ya kuanzia jitihada hizo.