Elections 2010 Je, Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?

Elections 2010 Je, Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?

Nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2010-2015?

  • Jakaya Mrisho Kikwete (CCM)

    Votes: 591 23.9%
  • Willibrod Slaa (CHADEMA)

    Votes: 1,785 72.1%
  • Ibrahim Lipumba (CUF)

    Votes: 89 3.6%
  • Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi)

    Votes: 7 0.3%
  • Mutamwega Mugahywa (TLP)

    Votes: 7 0.3%

  • Total voters
    2,475
  • Poll closed .
Wadau,

Nimekuwa nikifuatilia mijadala inayoendelea katika forum hii. Nataka kutoa changamoto kwa wadau wenzangu ili tujadili swali lifuatalo:


Je, ni mtanzania gani ana SIFA na VIGEZO vya kuiongoza Tanzania? Wachangiaji wanaweza kupendekeza majina MATATU.


Itakuwa vyema kama wachangiaji watatoa sababu zinazowafanya watoe mapendekezo hayo?


Nawasilisha hoja:

UPDATE:

Majina Matatu (makubwa) Yaliyopendekezwa:


  1. Jakaya Kikwete - CCM
  2. Willibrod Slaa - CHADEMA
  3. Ibrahim Lipumba - CUF

dr slaa
 
You can fool people sometimes but you cannot fool them all the times. My fellow Tanzanians use your citizen right to vote for the presidency of your choice, whom you are sure that he will not compromise our nation and the dignity of Tanzanians.: llama:
 
Dr Slaa yes we can!
Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.


Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupunguzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!


Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendelee kuwa watumwa ni nini?


Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..


Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na longolongo za CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.


Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi?


CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!


Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Nani anabisha! Si tumeona alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekalia mawe? We must be serious!


Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu?


Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?


Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini kila leo rais kuwaabudu wazungu na bakuli la kuombaomba! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania. Ee Mungu utuhurumie!


Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie.


Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.

Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi.


Peleka ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Waambie Nyerere alikwishakufa na nchi imeishatekwa nyara na vibaka. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..
 
Wote waliopo kwenye kinyang'anyiro wanafaa ISIPOKUWA kwa mfumo wa katiba tuliyonayo hata awe muadilifu kiasi gani hili linchi litamshinda tu. Tuifumue hii katiba yetu kwanza tuiweke sawa halafu tupate kiongozi muadilifu tuone kama mambo hayatakwenda....
 
kiongoze mwenye nguvu ya kufanya maamuzi... NAMAANISHA AKITOA TAMKO KINACHOFUATA NI UTEKELEZAJI
 
Mgombea anaefaa kuwa Rais ni Dr. Wilbrod Slaa.
Sababu! Sere ya elimu Bure pamoja na kubadilisha Katiba na kupitia upya mikataba wa wawekezaji ili kuondoa aina yeyote ya ukandamizaji au wizi uliofanyika wakati wa kusaini mikataba hiyo.

Lema
 
Wadau,

Nimekuwa nikifuatilia mijadala inayoendelea katika forum hii. Nataka kutoa changamoto kwa wadau wenzangu ili tujadili swali lifuatalo:

Je, ni mtanzania gani ana SIFA na VIGEZO vya kuiongoza Tanzania? Wachangiaji wanaweza kupendekeza majina MATATU.

Itakuwa vyema kama wachangiaji watatoa sababu zinazowafanya watoe mapendekezo hayo?

Nawasilisha hoja:

UPDATE:

Majina Matatu (makubwa) Yaliyopendekezwa:

  1. Jakaya Kikwete - CCM
  2. Willibrod Slaa - CHADEMA
  3. Ibrahim Lipumba - CUF

Uongozi ni kazi ngumu, ni kazi inahitaji muda na kujitoa kweli kweli katika kuhakikisha kwamba Taifa linafika kule ambako wote kwa pamoja tunaamini ni muhimu taifa lifike. Maeneo ambayo kwa pamoja kunamakubalino bila kujali ni nani anachanganua vizuri zaidi ni kama yafuatayo:-
1. Wote tunahitaji huduma bora za jamii-huduma hizi ni Afya, Elimu pamoja na miundombinu bora katika nchi yetu. Miundombinu hapa ni barabara, njia za reli n.k
2. Wote tunahitaji uchumi unatoa fursa kwa watanzania kuumilki. Tunataka uchumi ambao kukua kwake kunamnufaisha moja kwa moja mtanzania bila kujali kwamba yuko kwenye kundi gani la jamii ya watanzania. Uchumi unaotoa fursa sawia kwa kila mwenye kuthubutu kufanya kazi kwa akili na kwa kujituma. Kwa pamoja tunataka kuona uchumi ambukizi kutoka juu kwenda chini ( Economic multiplicity).
3. Wote kwa pamoja tunakubalina kwa namna fulani kwamba maliasili tulizonazo zinatosha kuiendesha inchi na kuwasaidia Watanzania kupata huduma muhimu ambazo wanataka. Misitu yetu, Milima yetu, Wanyama wetu , Bahari na maziwa na vyote tulivyonavyo kama malia ya asili vitumike kuleta neema kwa Watanzania.
Ili kufanya haya tunayo kubalina kwa pamoja kwa namna fulani kuwa kwa faida yetu sote tunahitaji kiongozi wa sifa zifuatazo:-

1. Kiongozi mwenye maono ya Tanzania ipi tunaitaka hapo baadaye. Kiongozi ambaye anaiangalia Tanzania kwa miaka mingi ijayo. Kiongozi huyu atoe dira ya Taifa letu lijalo na awe tayari kusimamia hilo
2. Kiongozi mwenye kuthubutu kufanya maamuzi magumu, haijalishi kwamba anaweza kukosana na wenzake lakini awe ni kiongozi mwenye kuthubutu kuamua njia ya kufuata na kupambana na hali yoyote ile kwa manufaa ya Taifa lake. Uongozi ni kujitoa mhanga kwa ajili ya Taifa kwa gharama yoyote
3. Kiongozi mwenye, wa kukemea, kuonya, kufundisha, kuelekeza na kuelimisha wengine wapi Taifa lipaswa kwenda kwa juhudi zake mwenyewe.

Kutokana na sifa hizi, ninashawishika, nijiaminisha na kujisaidikisha kwamba Dr. Willibroad Peter Slaa kwa juhudi na maarifa yake binafsi amethubutu kuzitafuta sifa hizi za kiongozi bora. Sifa hizi amezipata kwa kujibidisha kwake katika kujifunza kwa kusoma sana, kutafuta kwa njia ya kutafiti sana kila analotaka kusema na kulichangia, kujitoa kwa kuthubutu kusimama pekee yake katika kile anachoamini kwa kukemea, kuelimisha, kushawishi, kuonya n.k bila kuhofu kwamba atatengwa na wenzake kwa kufanya hivyo amelisaidia Taifa kuwa katika mwerekeo mpya kisiasa tulionao sasa. Sifa hizi hana Jakaya Mrisho Kikwete wala Ibrahimu Haruna Lipumba. Sifa hizi za Dr.Slaa hazifuati dini bali ni sifa za mtu binafsi kutokana na bidii ya kujitafutia maarifa na ufahamu lakini pia kuwa tayari kufa kwa kusema ukweli. Tanzania imeharibiwa kiutawala kupitia viongozi wa kisiasa tunahitaji kiongozi makini sasa ili kuiondoa nchi katika umaskini tuliomo na uzembe unao endelea katika utendaji wa maisha ya kila siku. Dr.Slaa anaweza kuwa sehemu ya kuanzia jitihada hizo.
 
"Let us not be content to wait and see what happen.But give us the determination to make the right things happen"
we were fooling for a long period now.itz our time to change facts into values,to choose a talented and the one that can fled us from Egypt 'a slave land' to Canaan.
***Dr. Slaa is the one to choose for the liberation of this nation***
The day will come........
To have a 2nd indepent in our societies
 
Naungana nawe mheshimiwa. tungekuwa kwa mfano na bunge linalofanya kazi bila kujali maslahi ya chama madudu haya yote aliyoyafanya raisi wetu sasa hivi asingekuwepo madarakani
 
watanzania wakubali mabadiliko! tatizo kila kiongozi anayekuja hana mfumo mzuri wa uchumi hivyo hawana jipy ila mabadiliko huja taratibu, watanzania waanze kwa kukubali kuwa bila CCM iNAWEZEKANA HIVYO ni muda mwafaka sasa wa kukabidhi madaraka kwa chama cha CHADEMA!
 
Ni Dr. Slaa. Sera na mikakati ya Dr. SLAA na CHADEMA kwa ujumla kweli itaturudishia hesima ya kufanya kazi kwa bidii huku tukifuata sheria na taratibu za nchi yet. Mwisho wa ufisadi na ubabaishaji
 
hapo sasa,tatizo CCM imegeuka ufalme sio chama tena, kila utakachoona kinafaa kukirekebisha chama lazima mfalme (Kamati Kuu) akikubali laasivyo unaambiwa kaa usubiri kwanza
 
Tembeeni nchi za wengine muone walivyo na maendeleo. sio hapa kwetu tunacheza tu. Hatuna viongozi kabisaaaa. Turudishe wakoloni basi. wanang'ang'ania tu.
 
We actually need a president, who can spearhead proper solutions to all Tanzanians Prolems......With utmost good faith,first degree loyalty to fellow humane Tanzanians,as well as oneself ! Tanzanians need to be sure ,to predict what comes,for their futures sake ! It requires no diplomas to phase out what comes out of the unpredictable candidates.......... I have looked closely ,through the whole list of the Tanzaians ,who have fulfilled the requirements for the race ,and came out concluding none of the candidate, is as properly deployed as is Kikwete. I hope Tanzania start again cruising,this time faster, Aboard that ship called Success for all Tanzanians,With Kikwete commandeering the outfit.
 
I beg to differ! Kikwete has quite the opposite of the characteristics you have referred to him:
We actually need a president, who can spearhead proper solutions to all Tanzanians Prolems......With utmost good faith,first degree loyalty to fellow humane Tanzanians,as well as oneself !

  • Kikwete has shown that he has utter disregard for Tanzanians as he has embraced and colluded with people who has skinned this country dry. EPA, MEREMETA, Richmond, only to mention a few.
  • Nepotism has become part and parcel of his governance. Note the Kikwete, Kingunge, Makamba, etc names in public forums as being leaders of this country.
  • Rampant misuse of governments' money

Tanzanians need to be sure ,to predict what comes,for their futures sake ! It requires no diplomas to phase out what comes out of the unpredictable candidates.......... I have looked closely ,through the whole list of the Tanzaians ,who have fulfilled the requirements for the race ,and came out concluding none of the candidate, is as properly deployed as is Kikwete. I hope Tanzania start again cruising,this time faster, Aboard that ship called Success for all Tanzanians,With Kikwete commandeering the outfit.
 
Anayetufaa kuwa Rais wetu watanzania ni yule tu ambaye ni mpya katika duru za kisiasa, mwenye damu mpya ya siasa na ambaye hana hata chembe ya shutuma toka kwa wananchi ukilingnisha na hao wengine.Huu sasa si wakati wa kuangalia umaarufu wa majina au vyeo vya kisiasa bali ni wa kati wa kufanya maamuzi ya hekima na busara. Kwa maoni yangu ndugu HASHIM RUNGWE, ndiye anayefaa kuwa Rais na si hao manyang'au. Wamezingirwa na kashifa kila upande kuanzia rushuwa hadi mambo ya kiutu uzima.
 
Back
Top Bottom