Elections 2010 Je, Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?

Elections 2010 Je, Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?

Nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2010-2015?

  • Jakaya Mrisho Kikwete (CCM)

    Votes: 591 23.9%
  • Willibrod Slaa (CHADEMA)

    Votes: 1,785 72.1%
  • Ibrahim Lipumba (CUF)

    Votes: 89 3.6%
  • Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi)

    Votes: 7 0.3%
  • Mutamwega Mugahywa (TLP)

    Votes: 7 0.3%

  • Total voters
    2,475
  • Poll closed .
2010 -2015 Edward Lowassa anafaa sana ndani ya CCM..JK angekuwa na busara ya kumwachiaa ili angalau kuwe na kautekelezajii katika mipango ya serikali.
 
Rais kwa CCM tutapoteza muda tu jamaa wamekwishamaliza uteuzi wao. Upinzani akitokea DR. Silaa na akapata support ya kutosha kutoka vyama vingine vya upinzani itakuwa safi sana maana anauzika . Lakini iwayo yote tukimpata Mtu kama J.P. Magufuli kulia kwa Rais kama kiranja mkuu (PM) pia inafaa saaaaaana. Tunahitaji mtu wa kuwaamsha watendaji wa serikali kutoka kwenye usingizi wa pono waliolala.
 
Jamani nchi hii kwa kweli lazima tukubaliane CCM wakati wao umekwisha,tangu 1977 hakuna jipya walilolifanya na hakuna hata kiongozi mmoja wa CCM anaefaa kutuongoza kwa sasa kwa sababu kama angekuwepo basi tungeshamuona kajiondoa kabisa CCM na kuhamia upinzani.
nadhani kiongozo yoyote wa upinzani anafaa cha muhimu ni kuliondoa hili jinamizi CCM,watanzania amkeni kama wenzetu wa kenya,zambia,malawi,waliamua kwa pamoja kuvitokomeza vyama hivi viovu.tuweke cha chochote cha upinzani ili nchi yetu iwe sawa.naamini maneno ya wengi kuwa Viongozo wote waliopata kuingoza nchi hii si watanzania halisi.
Dr.Slaa unafaa,Dr.Salim unafaa.
Mungu ibariki TANGANYIKA
 
Sidhani kwamba Kikwete anafaa kwa namna yeyote ile. Kumbuka hata kama Waziri Mkuu ni mzuri kiasi gani wanaoendesha nchi ni wale mafisadi ambao wala hawana vyeo hivyo JK No way!!!! Kama ni JK na John Shiduba (JS) mara mia ukampa JS angalau kwa ajili ya mabadiliko.
 
Dr Slaa, nakuona hapa, nakuomba uje ujibu tena maswali yetu hapa kama ulivyofanya huko nyuma.
 
Hakuna anayefaa. Tunahitaji mtu mwenye vision, atuondoe usingizini na kututoa kwenye visingizio vingi tulivyo navyo on our poverty.
Hakuna anyefaa maana ili uweze kufikia mahali pa kuwa mgombea urais utakuwa umevuka mizengwe mingi hivyo bila shaka utakuwa nawe ni mtu wa mizengwe. Dk Slaa na wenzake wanaweza kuwa wazuri sana kukosoa lakini wakashindwa kuongoza.Next tuna matatizo ya kukumbatia uwongo na porojo sijui imekuwa ni culture yetu?.We need leadership ku shake up the whole system and 'culture'.
 
Wapo wengi wanaofaa lakini tatizo kubwa ni wapiga kura wasiofaa wanapomchagua asiyefaa. Kwanini mtu anunuliwe kwa bei ndogo tu ya wali hatimaye anakwenda kumchagua mtu?Wapiga kura wanaofaa wasipopatikana ni shida zaidi kumpata anayefaa.
 
917154]Hakuna anayefaa. Tunahitaji mtu mwenye vision, atuondoe usingizini na kututoa kwenye visingizio vingi tulivyo navyo on our poverty.[/COLOR]
Hakuna anyefaa maana ili uweze kufikia mahali pa kuwa mgombea urais utakuwa umevuka mizengwe mingi hivyo bila shaka utakuwa nawe ni mtu wa mizengwe. Dk Slaa na wenzake wanaweza kuwa wazuri sana kukosoa lakini wakashindwa kuongoza.Next tuna matatizo ya kukumbatia uwongo na porojo sijui imekuwa ni culture yetu?.We need leadership ku shake up the whole system and 'culture'.

Kwako bwana mdogo anayefaa ni nani? kusisitiza tu hakuna anayefaa haitusaidiii! huyo unayeona ana vision ni nani maanake umesisitiza hakuna anayefaa bila kutupa huyo unayedhani anafaa!
 
2010 -2015 Edward Lowassa anafaa sana ndani ya CCM..JK angekuwa na busara ya kumwachiaa ili angalau kuwe na kautekelezajii katika mipango ya serikali.
Vichekesho sana.. Makosa makubwa ya JK ni kuwa baba huruma kwa majambazi kama kina Lowassa, Mahita, Chenge na wengineo. Sasa ajabu ya Firaun ni kwamba ule ukatili na ujambazi wao ndio watu wanaona ni Ujasiri na wachapakazi..Pengine tuongezee kusema Lowassa rais na Mahita waziri mkuu.
Kaaazi kweli kweli!
 
Tunapo taja majina haraka haraka ndipo tunapo kosea. Kwanza tuna takiwa kuainisha sifa na vigezo vya raisi tunaye hitaji(msisitizo kwenye tunaye mhitaji siye tunaye mtaka). Baada ya hapo ndipo tuangalie kati ya viongozi wata kao jitokeza kuomba kura zetu nani ana timiza hizo sifa na vigezo zaidi ya wengine? Tuna bidi tuku bali kwamba chaguo la raisi wetu lina kuwa ni short list iliyo andaliwa na vyama vyetu vya siasa kwa hiyo siyo lazima tunaye mtaka awe raisi ana taka kuwa raisi au ana kubalika kwenye chama chake.
 
Kwanini tusichague tuu! mradi tu anatufaa!

hata hao wanaokubalika kama viongozi wa Chama, chagua tu!
Tunahitaji Raisi au kiongozi anayehitajika sasa- kama mwanafalsafa-anatakiwa Kiongozi !
 
JK as a person is really good chap. Lakini as the President i really doubt.

Angalia alichukua nchi ikiwa katika hali gani kiuchumi, look at it now. Inflation ilikuwaje alipochukua nchi, it was very low, look at it now tunaelekea kwenye inflation inayofanana na nchi ambazo hazimanage uchumi wake vizuri, we are very close to that.

Angalia utekelezaji wa Sheria na haki. Wenye nguvu na wenye pesa ndio wenye haki, wanyonge hawana haki. Mfano mzuri ni kesi ya Ditopile, na kesi ya EPA etc...justice serves the rich. Wezi wa mabilioni wanafahamika wapo tu wanapeta na wanajidai na ulinzi juu na wanatumia raslimali za serikali, mhasibu mmoja aliiba laki 2 huko moshi sasa yuko ndani.

Angalia kama kuna any sound social and economic plan, au hata supervison na implementation ya mipango ya serikali ya awamu ya tatu, hakuna kitu ambacho mtu mwenye akili timamu atakubaliana nacho.

Nothing tangible that his government can show.

Lakini kama ukiniwekea Lowassa na JK, i will go for JK, ukiniwekea JK na Kingunge i will go for JK, so it depends kama CCM watakuwa makini kuweka watu watakao mchallenge JK. Na kwa upande wa pili inatagememea nani kutoka opposition atasimama, kama ni Mrema bado by far unaona ni afadhali JK.

Wanaompigia debe JK wanafanya hivyo kwa jili ya interest zao binafsi, na sio kwa kuwa JK anafaa kuwa rais, we all know that the chair is too big for him.
 
Tunapo taja majina haraka haraka ndipo tunapo kosea. Kwanza tuna takiwa kuainisha sifa na vigezo vya raisi tunaye hitaji(msisitizo kwenye tunaye mhitaji siye tunaye mtaka). Baada ya hapo ndipo tuangalie kati ya viongozi wata kao jitokeza kuomba kura zetu nani ana timiza hizo sifa na vigezo zaidi ya wengine? Tuna bidi tuku bali kwamba chaguo la raisi wetu lina kuwa ni short list iliyo andaliwa na vyama vyetu vya siasa kwa hiyo siyo lazima tunaye mtaka awe raisi ana taka kuwa raisi au ana kubalika kwenye chama chake.

Kweli, tuweke sifa kwanza, halafu tuangalie nana anaendana nazo, halafu ni mambo gani amefanya kwa moyo na kwa maslahi ya taifa ili kujenga imani - kashfa moja tu nje ya ulingo!
 
Salim Ahmed Salim anatufaa sana kutokana alichokwisha kifanya kwa taifa letu akiwa kama waziri mkuu, waziri wa ulinzi n.k. Diplomasia ya ulimwengu anaifahamu vizuri sana. Kuna viatu vilikwisha pewa jina lake enzi zile watu walikosa viatu na kuvaa matairi ya gari, watu walikosa kabisa nguo na kuvaa magome ya miti alijitahidi kumwelewesha Mwl. JK na kuingiza mitumba kwa utaratibu mzuri sio ule wa mzee ruksa wa kuleta mpaka chupi!

Waziri mkuu John Pombe Maghufuli - amegundua wizi wa samaki toka miaka ya 70 wakati eti tuna jeshi la wana maji pale Kigamboni, kajenga barabara nyingi na kuwaadabisha wakandarasi waliokiuka mikataba, kafunua uozo wa wizara ya ardhi na kuwa jasiri kumtaja Lita, naibu waziri wake kuwa naye anahodhi viwanja kibao. Watu tunao lakini shida ni mfumo wa vyama ndio maana wanaogopa mgombea binafsi na CCJ ambao watawapokea CCM wanaokubalika na kuchukua nchi na kuwatia adabu akina JK, Tendwa, Marmo, Kingunge n.k.
 
Tatizo linalotukabili sasa hivi hatuna wale "King Makers "wa kweli. Kwa Mfumo tuliokuwa nao mtu ambaye hayupo kwenye Mtanadao ni vigumu kupenya sababu wapiga kura hawaelewi jinsi ya kuchagua na ukichangia hali yao ya umasikini it makes even worse. Tujaribu kuelimisha watu waelewe matatizo yao yataondokaje. Kiongozi tunaemhitaji sio tuu katika ngazi ya Urais bali katika kila ngazi ni yule Mkweli atakaewajali na kuwasikiliza wale anaewaongoza na maamuzi yao yawe ya pamoja kwa kukubaliana. Unaweza kumuona Kiongozi anaefaa kutokana na matendo na tabia zake za awali na mwenendo wake wa maisha.
Hatuhitaji kumuweka mtu madarakani kwa kuhisi labda atafanya mazuri baada ya miaka kumi watu watakuwa wameshachoka na wengini kufa kwa umasikini na hali mbaya ya umasikini.
Challenge kubwa ni je yupo mtu wa namna hiyo kutokana na wale tuliozoea kuwaona?
 
Natumaini wakati umefika tukaondokana na wazo la kuongozwa na CCM. Ni miaka takribani 50 sasa toka nchi yetu imepata uhuru toka kwa wakoloni na chama kilichoongoza muda wote huo ni CCM na hakuna maendeleo yoyote ya kujivunia kama nchi huru. Huduma za za jamii zinazidi kudorora: shule,upatikanaji wa maji safi,matibabu na hata mkulima hana uhakika wa wapi atauza mazao yake na kupata pesa za kuweza kurudisha gharama zake na yeye kubaki na ziada. Nafikiri wakati umefika kuuelimisha umma kuwa umasikini wao na shida zao unaletwa na CCM kwa hiyo tufanye mabadiliko ya maana kwa faida yetu sote.
 
Katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge utakaofanyika October mwaka huu tuna wagombea wengi ambao hadi hivi sasa wameshajitokeza kuwania nafasi ya urais wa nchi. Nafikiri tujaribu kuangalia ni nani atafaa kuwa Rais wa Tanzania kati ya hawa wengi waliojitokeza na kwanini tunafikiri atatufaa. Ni rukhusa kuandika sifa zote ambazo tunazitaka kwa Rais wetu na kuelezea ni nani anazo na nani hana. Ukiweka na sababu kwanini anazo au hana, itapendeza zaidi.
Karibuni tuchangie na tupige kura.

Waliojitangaza hadi sasa ni
Jakaya Kikwete
Wilbroad Slaa
Ibrahimu Lipumba
Mutamwega Mugahywa na
Rungwe
Kama kuna anayemiss mnaweza kuongeza
 
Katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge utakaofanyika October mwaka huu tuna wagombea wengi ambao hadi hivi sasa wameshajitokeza kuwania nafasi ya urais wa nchi. Nafikiri tujaribu kuangalia ni nani atafaa kuwa Rais wa Tanzania kati ya hawa wengi waliojitokeza na kwanini tunafikiri atatufaa. Ni rukhusa kuandika sifa zote ambazo tunazitaka kwa Rais wetu na kuelezea ni nani anazo na nani hana. Ukiweka na sababu kwanini anazo au hana, itapendeza zaidi.
Karibuni tuchangie na tupige kura.

Waliojitangaza hadi sasa ni
Jakaya Kikwete
Wilbroad Slaa
Ibrahimu Lipumba
Mutamwega Mugahywa na
Rungwe
Kama kuna anayemiss mnaweza kuongeza


anayefaa ni Jakaya Mrisho kkikwete
 
Anayeweza hii kazi ni wps.
Sababu zipo nyingi.1 ni mzalendo
2 ni mkweli.
3ni msomi [dakta wa ukweli].
4 ameonyesha anaweza alipokuwa bungeni.
5 anajuwa ni kwa nini nchi yetu ni masikini pamoja na kuwa na rasilimali kibao.
6 hamwogopi mtu.
7 si rahisi kuwekwa mfukoni na mafisadi.
8 anafanana na mwalimu [hajajilimbikizia mali.
9 hakurupuki kweye hotuba zake.
10 walio mzunguka kwenye chama chake nao ni wazalendo.
11 anawajua mafisadi wote wanao itafuna nchi yetu.
12ameonyesha anaweza kupunguza matumizi makubwa ya serikali yetu.
13 ndio suluhisho la matatizo ya wafanyakazi
13 ......................
14 ....................... Yaani zipo nyingi sana.
 
Back
Top Bottom