Je, mtoto mchanga akiwa tumboni kwa mama yake anaweza kuugua?

Je, mtoto mchanga akiwa tumboni kwa mama yake anaweza kuugua?

LAMBOFGOD

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2016
Posts
1,561
Reaction score
1,319
Wana JF karibuni kwa mjadala huu

Napenda kujua kama watoto wachanga wawapo tumboni kwa mama zao {kabla ya kuzaliwa} wanaweza kuugua {ugonjwa wa aina yeyote}?

Na kama huwa wanaugua nini hutumika kama dawa kuwaponesha? Au mechanism gani hutumika kumponesha kutoka kwa mama yake?

Na kama hawaugui wawapo tumboni takribani miezi tisa kwa nini mara tu wazaliwapo na kuanza kuishi huku duniani huandamwa na magonjwa tangu utoto hadi umati?

Magonjwa yanaexist katika ulimwengu gani?

Na kama hawaugui je dawa tunazotumia ni sahihi kwa miili yetu?
 
Huugua na kufa pia, na mama akinywa dawa ambayo itapenya kwenda huko kwa mtoto basi yaweza mdhuru pia, mf anaweza zaliwa hajakamilika au hata akawa kilema, magonjwa ambayo mtoto akiugua akiwa tumboni hujionesha mtoto akizaliwa mfano wake ni virus vya ukimwi, syphillis nk... kama una swali uliza zaidi
 
ndio wanaugua, ndio maana mama mjamzito hukatazwa baadhi ya tabia/vitendo maana huweza sababisha mtoto kuzaliwa na matatizo (kuuguli ndani kwa ndani hadi kukata moto)
 
Wana JF karibuni kwa mjadala huu

Napenda kujua kama watoto wachanga wawapo tumboni kwa mama zao {kabla ya kuzaliwa} wanaweza kuugua {ugonjwa wa aina yeyote}?

Na kama huwa wanaugua nini hutumika kama dawa kuwaponesha? Au mechanism gani hutumika kumponesha kutoka kwa mama yake?

Na kama hawaugui wawapo tumboni takribani miezi tisa kwa nini mara tu wazaliwapo na kuanza kuishi huku duniani huandamwa na magonjwa tangu utoto hadi umati?

Magonjwa yanaexist katika ulimwengu gani?

Na kama hawaugui je dawa tunazotumia ni sahihi kwa miili yetu?
anaweza kuugua
 
anaweza kuugua na kupoteza maisha kabisa...mfano wa magonjwa ni malaria,kaswende,magonjwa ya moyo nk
 
Ndio Anaweza.

Kuna kitu kwa lugha ya watu weupe kinaitwa Vertical Transmission, uambukizaji wa magonjwa toka kwa Mama kwenda kwa mtoto, hii hutokea kupitia placenta.

Mara nyingi magonjwa yanayoambukiza kwa njia hii ni kama Trachoma (matatizo ya macho), Kaswende, Malaria n.k

Lakini pia mtoto anaweza kupata maradhi akiwa ndani ya tumbo la Mama na kutoka na matatizo ya kimwili au kupelekea kupoteza uhai wake angali tumboni au punde tu Mara baada ya kuwasili duniani (kuzaliwa), Maradhi/Matatizo hayo husababishwa na madawa, matumizi ya vilevi, n.k
 
Back
Top Bottom