Je, mtu anaweza ambukizwa magonjwa ya zinaa bila kufanya ngono?

sinachangu

Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
47
Reaction score
17
Kiukweli hili jambo lanichanganya sana. Mtu waweza pata magonjwa ya zinaa kama kaswende na mengineyo hata kama hujafanya ngono?

Hii ni mara ya pili napimwa naambiwa nina magonjwa ya zinaa hali ya kuwa sikushiriki tendo la ndoa. Je, madakatari na wengineo mtu anaweza kuambukizwa magonjwa ya zinaa bila ya kushiriki tendo la ndoa na mtu yeyote? kama ndio kivipi?

Asanteni, naombeni ufafanuzi zaidi.
 
bila ku-du unamanisha nin usije ukawa hau du ila unashiriki oral sex???
 
Hiyo abstinence ni ya kipindi gani? Una uhakika ni total abstinence? Hayo magonjwa 'uliyokutwa' nayo ni yapi au ni ugonjwa upi? Acha kusema eti magonjwa kama Kaswende na mengineyo, sema ugonjwa uliotajiwa hapo ulipopima maana hauna sababu ya kuogopa kutaja ugonjwa 'provided' haujatutajia jina lako maana kwa kutaja ugonjwa najua itakuwa rahisi kwa wataalam kukueleza kama unaweza kuupata kwa njia nyingine tofauti na kujamiiana.

Muhimu kuzingatia historia uliyotoa maana maeneo mengine hawapimi, wakishasikia malalamiko yako yanaendana na mwelekeo wa kaswende na wakikutathmini wakaona unaelekea 'unapiga game' mara kwa mara wanaunganishia juu kwa juu (which is wrong anyway).
 
Mkuu Utotole nilipima mwaka 2011, nikaambiwa nina kaswende. Nikatumia dawa mpaka nikamaliza doze. Juzi tena nimeumwa tumbo chini ya kitovu, homa kali na maumivu wakati wa kutoa haja ndogo. Nimepimwa nimeambiwa nina ugonjwa wa zinaa. Sikuwauliza ni ugonjwa gani, nachanganyikiwa na hayo majibu yani.Muda wote huo sikushiriki game lakini ndio hivyo napatwa na hayo magonjwa. Na hiyo abstinence, ni total abstinence.
 
Last edited by a moderator:

Ndiyo inawezekana kabisa kwa mtu hususani KE kupata magonjwa ya zinaa pasipo hata kushiriki tendo la ndoa. Kwa mwanamke anaweza akaambukizwa gonjwa la zinaa mfano kaswende au kisosono kwa kupitia kutumia sehemu za kujisaidia ikiwa ni vyoo vya kukaa na vyombo vya kujitawadha iwapo hali ya usafi wake utakuwa duni. Mwanamume japo naye anaweza kuambukizwa kupitia njia hizo uwezekano ni finyu sana. Ila kwa KE uwezekano ni mkubwa sana. Wanawake wanapaswa kuwa makini sana na usafi wa vyoo jumuiya(public toilets). Na inapowezekana waepuke kutumia vyoo hivyo na vyombo vya kujitawadha na inapowalazimu kutumia public toilets watumie kwa tahadhari.
 
Mkuu samahani japokuwa swali langu halitakusaidia...ina maana tangu 2011 huja... kabisa!!??? Una umri gani mkuu na jinsia gani?!
 

Asante sana mkuu kwa ufafanuzi wako mzuri. Hakika nimejifunza.
 
Hukupata karatasi yoyote yenye matokeo yavipimo vyako?
Ni very rare kupata ugonjwa wa zinaa bila kufanya ngono, kinachoweza kuwa kimetokea ni vipimo vimekosewa (kawaida sana na vipimo vyetu) au ulikuwa haujapona kabisa mara ya kwanza na virus ilikuwa imejificha mwilini. Nakushauri utafute second oponion ya kitaaalamu.
 

Asante kwa ushauri wako. Hata hiyo mara ya kwanza niliambukizwa bila kufanya ngono. Nitafanya vipimo tena baada ya kumaliza dose.
 
kuna uwezekano tena mkubwa tu but according ninavyoelewa mimi,,,,kwa mfano kama ugonjwa wa zinaa uitwao candidiasis waweza pata whithout sex kwa sababu kuna wadudu walinzi wa magonjwa kwa mfano kuna commensal mmmoja anaitwa normal flora ambaye anaprotect from infection,,,,,so kuna sababu ambazo zinaweza kuchangia kwa huyu mdudu ambaye ni mlinz wa gonjwa la zinaa akabadilika akawa amebadilika akausababishia ugonjwa bila sex....mojawapo ya sababu zinazosababisha huyo mdudu achange ni kama @.local changes to the vaginal immunity kwa mwanamke @immunosuppresant disease or treatment eg AIDS,chemotherapy @Drug therapy eg antibiotics @Endocrine disease eg diabbetic mellitus @Physiological changes@Miscellaneous disorders eg Iron deficiency...kwa ushari uwe unapima mara kwa mara.ASANTE
 
Je ushawahi kuugua kutokana na kufanya ngono? Kama ulishawah kufanya ngono ukaupata then ukatibiwa halafu umejirudia tena pasipo kufanya ngono inawezekana mkuu
 
Lakin kama huhawah shiriki ngono ya aina yoyote tangu ubalehe haiwezekani
 
Ukichangia taulo na mwenye kaswende unaweza pata maumbukizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…