Je mtu anaweza fungua kesi ya madai katika hili?

consigliori

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2010
Posts
392
Reaction score
89
Ndugu wanasheria, naomba nisaidiwe kwenye suala hili hapa chini;

Nilifanya inteview ya kazi ( 4 rounds) kwa mwajiri fulani, na akanitaarifu kuwa nimeshinda na kwa hiyo nipange lini tukane kwa ajili ya negotiations za offer.

Baadaye, kabla ya kukutana kwa ajili ya kujadiliana kuhusu hiyo offer, nikaambiwa ati, wameambiwa na HQ yao kuwa kabla ya kunipa offer, inabidi niwe interviewed na afisa mwingine ( yaani round ya 5 ambayo haikuwepo katika utaratibu wa mwanzo).

Je? nina haki yoyote ninayoweza kuidai mahakamani ikiwa mwisho wa siku sitaipata hiyo kazi?

Asante
 
Unataka udai nini sasa?
Sina hakika mkuu, ndo naomba wenye macho ya kisheria mnishauri kwani naamini nitakuwa nimedhulumiwa kwa sababu mtihani nishafaulu, sasa kwa nini nifanyishwe mtihani mwingine?
 
1. kwani umeshajua matokeo ya round 5?
2. Unasababu yoyote ya kufikiri hautendewi haki?
3. unajua referee wako -kama wametafutwa wamesema nin? inaweza kuwa sababu pia.....

kimsing hata ukishapewa offer bado kuna probation period within which eather side can terminate contract

HUNA CHA KUDAI.
 
 
Ungesubiri ufanye hiyo interview ndiyo uombe ushauri. Sasa kwa hali ilivyo inawezekana wameshasoma hata huu uzi kwani hii case ni unique! Next time be patient.
 
Huna contract, utashitaki nini? Uko kwenye stage ya interview, hata offer haijawa accepted, there is nothing to claim
 
Aisee kumbe ni wewe ndiyo natakiwa kukufanyia usaili? Sasa kwa nini umekuja huku kulalamika?? Ulishindwa kupiga simu na kuuliza sababu kwetu??

Anyway haina shida, tuonane kwenye usaili tutaongea vizuri.
 
1. Kila mwajiri ana sheria na taratibu ambazo taasisi inajiwekea katika kutoa huduma. Na hata suala la kuajiti ikiwa ni pamoja na utaratibu wa interview wanajiwekea. Baadhi ya waajiri hata interview huitaji kwa kutegemea CV yako ilivyosimama.
kwa sababu za ushindani, waajiri wanasuumwa kwenda mbele zaidi ya CV Hii ikiwa ni pamoja na kutaka walioomba wafanyiwe interview, au wafanye presentation baada ya interview.

Wengine wanaitisha interview zaidi ya moja na wengine wanakua na nterview written and oral.

SWALI:
1.Wewe unahisi umedhulumiwa au hujatendewa haki, ipi sasa!
2. Unaendeshwa na hisia zaidi kuliko hali halisi!
3. Usituhumu bila kuwa na sababu za msingi za kutuhumu, hasa sababu zako zikiwa wewe mwenyewe huwezi kuzitetea.
4. Unaonekana unataka ku- shoot before you are shot! its natural strategy but uwe mwanagalifu utachekesha
5. Positive descrimination ni aina ya utaratibu ambao unawapa nguvu waajiri katika kuendesha zoezi la kuajiri. Tough luck if you are the victim!

Bila kufuata utaratibu na sheria za mwajiri na kutimiza mahitaji ya mwajiri ni vigumu kujua kama mwajiri amekosea wapi???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…