Je! Mungu ni yule yule?

Je! Mungu ni yule yule?

MUNGU hajabadilika, ni Yule Yule, jana, leo, na kesho. Kilichobadilika ni Sheria za MUNGU na siyo AMRI za MUNGU. Kuna tofauti kubwa kati ya Sheria na Amri.

Wakati ule wa Agano la Kale, MUNGU alikuwa analiandaa taifa la Israeli ili kupitia taifa hili, Mwokozi wa ulimwengu mzima azaliwe. Ifahamike kwamba wakati ule wanadamu walikuwa kwenye ujinga wa hali ya juu sana wa kutomtambua wala kumkubali MUNGU. Hivyo basi hata yeye ilibidi awe mkali zaidi ili watu waweze kufahamu uwepo wake na ndiyo maana akaweka Sheria kali ili kila anayevunja sheria hizo, kama ni kufa na afe ili wengine wajifunze. Na ndiyo maana utaona hata wakati anawatoa wana wa Israeli pale Misri, alitumia nguvu kubwa na maajabu makubwa ili wanadamu wafahamu kuwa yupo MUNGU WA KWELI. Hata baadhi ya Waisraeli walipokosea wakati wakiwa jangwani, wakati mwingine alikuwa anawazamisha chini ya ardhi na kuwafukia wakiwa hai ili wale wanaobakia watambue kuwa yupo na wasirudie makosa kama yale. Tena akaweka Sheria kali na kuwakabidhi Makuhani Walawi wazisimamie na kuwaadhibu wale wote watakaozivunja Sheria hizi kwa namna Sheria inavyotaka.

Sasa basi utaona baada ya kuzaliwa kwa YESU KRISTO, sheria zilibadilishwa na MUNGU mwenyewe kupitia YESU KRISTO sababu mpaka wakati wa Agano Jipya tayari MUNGU wa KWELI alikuwa anajulikana isipokuwa tu baadhi ya watu walikuwa hawamtii, lakini kujua kama MUNGU yupo, walikuwa wanajua sana. Lengo la MUNGU lilikuwa ni kumleta Mwanawe duniani ili aje aikomboe dunia kutoka kwenye dhambi na hilo lilipofanikiwa, basi MUNGU akawaacha wanadamu wote na Waisraeli wachague wenyewe njia ya Wokovu au njia ya Upotevu. Akawaacha pasipo kuwaadhibu kwa kutumia Sheria kama ilivyokuwa enzi za Agano la Kale ambapo walikuwa wanaadhibiwa kwa kutumia Sheria.

Ndiyo maana ukisoma kwenye Biblia utaona kuna mahali YESU anasema; "sijaja kuitangua torati wala manabii, bali kuitimiliza". Na tena kuna mahali YESU anasema "maneno yangu siyo yangu bali ni yake Yeye aliyenituma". Hivyo basi tunaona kwamba MUNGU alimtuma YESU aje awafundishe wanadamu wasihukumiane tena, bali wawe wenye upendo na wenye kusameheana wao kwa wao na kuvumiliana mpaka siku ile atakapoleta hukumu kwa watu wote. Na ndiyo maana YESU aliwaambia Mafarisayo maneno haya; "enendeni mkajifunze maana ya maneno haya; nataka Rehema na siyo Sadaka". Hapa alikuwa anamaanisha kuwa anataka Mafarisayo na watu wote wawe na "huruma" zaidi kuliko kutoa Sadaka.

Ukitizama kijuu juu kwa macho ya kibinadamu, unaweza ukasema MUNGU amebadilika, lakini siyo kweli, MUNGU ni yule yule, isipokuwa tu amebadili Sheria na kuzifanya kuwa Neema yenye Upendo ili huruma yake kwa wanadamu aliyokuwa nayo tokea mwanzo ijidhihirishe kwa watu wa mataifa yote. Na ndiyo maana hata Mitume walisema kuwa "tunaokolewa kwa Neema tu", yaani, ni kama Zawadi tu, hatukustahili kuokolewa. Mfano mzuri ni enzi zile mtu akizini, alikuwa akikamatwa anazini, ilikuwa ni lazima auawe kwa kupigwa na mawe. Na hivi ndivyo sheria ilikuwa inataka iwe. Lakini utaona kwenye Agano Jipya, yule mwanamke mzinzi anapokamatwa na kuletwa mbele ya BWANA YESU, mwanamke yule anasamehewa na kuachiwa huru. Hii ndiyo "neema", yaani kwa neema tu anasamehewa ingawa Sheria inamuhukumu. Maana yake ni kwamba wale wasioipokea neema hii kwa kuacha dhambi zao, basi siku ya mwisho watahukumiwa kwa kutupwa kwenye moto kama Sheria inavyosema kuwa kila mzinzi, kama ni kufa na afe. Hivyo basi utaona "neema na rehema" zimepewa nafasi kipindi hichi ili watu wengi waokolewe, lakini wale watakaokataa kuzipokea rehema na neema hizi, hukumu ya moto inakuja juu yao.

MUNGU ni yule yule, MUNGU ni mkali sana, isipokuwa ni mvumilivu sana, tena anavumilia tu ili tuweze kujirudi na kuacha maovu yetu sababu hapendi hata mmoja wetu apotee. Hata yeye alisema kwa kinywa cha Nabii Isaya kuwa; "nimenyamaza kimya kwa muda mrefu, lakini sasa nitapiga kelele na kupaza sauti kama mwanamke aliye kwenye utungu wa kuzaa". Na kweli kabisa, sasa hivi MUNGU amenyamaza kimya, siyo kama zamani zile za Agano la Kale, lakini siku inakuja ambapo atapaza sauti yake, na hapo ndipo wanadamu na viumbe vyote watakapotambua hasira za MUNGU. Biblia inasema kuwa siku hiyo milima itakimbia na visiwa vitatoweka na mbingu zitafunguka kama vile mtu afunuavyo ukurasa wa kitabu. Siku ya ghadhabu na hasira ya BWANA MUNGU hakika inakuja.

Ndugu yangu RGforever MUNGU ni yule yule, jana, leo na kesho.
Nimependa sana maelezo yako Mungu akubariki atleast hapo nimeelewa
 
Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote, uoendo wote, kama mnavyomsema, kama yupo, pale alipoanza kuumba ulimwengu, alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao matetemeko ya ardhi yanayoua kwa kuzuka hai watoto wachanga hayawezekani kuwepo katika ulimwengu wake.

Hapa usiseme habari za shetani, dhambi etc. Hayo yote ni mambo ambayo, kwa mujibu wenu, yamekuja baadaye. Mwanzo Mungu alikuwa na uamuzi yawepo au yasiwepo.

Hakuumba ulimwengu huo ambao matetemeko hayo hayawezekani.

Ilikuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu unaoruhusu matetemeko haya, wakati alikuwa na upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote wa kuumba ulimwengu ambao matetemeko haya hayawezekani?

Hujajibu swali hili.
Sasa kama kaumba huo ulimwengu wenye shida ndio hayupo?
 
Kwa nini niamini hivyo? Kwa nini nithamini kuamini katika ulimwengu unaotaka kujua?

Kwa nini niamini contradiction?

Kwa nini niamini kuna pembetatu yenye pembe sita?

Hujaondoa contradiction katika idea ya kuwepo kwa Mungu wako.
Hujajibu swali
 
Kulingana na swali lako, ni yuleyule kwa binadamu wote? Mf. Aliyemtoa mwanae kafara na huyu wa Waislam ni yuleyule? Tuingie kipengele kimoja, wanaoamini Yesu ni Mungu, Wakatoliki na Wasabato wanaabudu Mungu yuleyule? Ni kwa nini kusiwe na kitu kimoja?
 
kuhusu mungu.ukweli ulio mchungu ni kwamba . sisi viumbe wake hatumjui.tunahisi tuu kwamba yupo miongoni mwetu.kazi na malengo yake haswaaa hatujayajua.tunamtafsiri ki dunia zaidi .wakati dunia ni moja ya mamilioni ya sayari za ulimwengu wake.kumbuka mungu wa wajinga ni tofauti na mungu wa werevu.
 
Back
Top Bottom