RGforever
JF-Expert Member
- Apr 3, 2011
- 6,878
- 5,432
- Thread starter
-
- #1,501
Nimependa sana maelezo yako Mungu akubariki atleast hapo nimeelewaMUNGU hajabadilika, ni Yule Yule, jana, leo, na kesho. Kilichobadilika ni Sheria za MUNGU na siyo AMRI za MUNGU. Kuna tofauti kubwa kati ya Sheria na Amri.
Wakati ule wa Agano la Kale, MUNGU alikuwa analiandaa taifa la Israeli ili kupitia taifa hili, Mwokozi wa ulimwengu mzima azaliwe. Ifahamike kwamba wakati ule wanadamu walikuwa kwenye ujinga wa hali ya juu sana wa kutomtambua wala kumkubali MUNGU. Hivyo basi hata yeye ilibidi awe mkali zaidi ili watu waweze kufahamu uwepo wake na ndiyo maana akaweka Sheria kali ili kila anayevunja sheria hizo, kama ni kufa na afe ili wengine wajifunze. Na ndiyo maana utaona hata wakati anawatoa wana wa Israeli pale Misri, alitumia nguvu kubwa na maajabu makubwa ili wanadamu wafahamu kuwa yupo MUNGU WA KWELI. Hata baadhi ya Waisraeli walipokosea wakati wakiwa jangwani, wakati mwingine alikuwa anawazamisha chini ya ardhi na kuwafukia wakiwa hai ili wale wanaobakia watambue kuwa yupo na wasirudie makosa kama yale. Tena akaweka Sheria kali na kuwakabidhi Makuhani Walawi wazisimamie na kuwaadhibu wale wote watakaozivunja Sheria hizi kwa namna Sheria inavyotaka.
Sasa basi utaona baada ya kuzaliwa kwa YESU KRISTO, sheria zilibadilishwa na MUNGU mwenyewe kupitia YESU KRISTO sababu mpaka wakati wa Agano Jipya tayari MUNGU wa KWELI alikuwa anajulikana isipokuwa tu baadhi ya watu walikuwa hawamtii, lakini kujua kama MUNGU yupo, walikuwa wanajua sana. Lengo la MUNGU lilikuwa ni kumleta Mwanawe duniani ili aje aikomboe dunia kutoka kwenye dhambi na hilo lilipofanikiwa, basi MUNGU akawaacha wanadamu wote na Waisraeli wachague wenyewe njia ya Wokovu au njia ya Upotevu. Akawaacha pasipo kuwaadhibu kwa kutumia Sheria kama ilivyokuwa enzi za Agano la Kale ambapo walikuwa wanaadhibiwa kwa kutumia Sheria.
Ndiyo maana ukisoma kwenye Biblia utaona kuna mahali YESU anasema; "sijaja kuitangua torati wala manabii, bali kuitimiliza". Na tena kuna mahali YESU anasema "maneno yangu siyo yangu bali ni yake Yeye aliyenituma". Hivyo basi tunaona kwamba MUNGU alimtuma YESU aje awafundishe wanadamu wasihukumiane tena, bali wawe wenye upendo na wenye kusameheana wao kwa wao na kuvumiliana mpaka siku ile atakapoleta hukumu kwa watu wote. Na ndiyo maana YESU aliwaambia Mafarisayo maneno haya; "enendeni mkajifunze maana ya maneno haya; nataka Rehema na siyo Sadaka". Hapa alikuwa anamaanisha kuwa anataka Mafarisayo na watu wote wawe na "huruma" zaidi kuliko kutoa Sadaka.
Ukitizama kijuu juu kwa macho ya kibinadamu, unaweza ukasema MUNGU amebadilika, lakini siyo kweli, MUNGU ni yule yule, isipokuwa tu amebadili Sheria na kuzifanya kuwa Neema yenye Upendo ili huruma yake kwa wanadamu aliyokuwa nayo tokea mwanzo ijidhihirishe kwa watu wa mataifa yote. Na ndiyo maana hata Mitume walisema kuwa "tunaokolewa kwa Neema tu", yaani, ni kama Zawadi tu, hatukustahili kuokolewa. Mfano mzuri ni enzi zile mtu akizini, alikuwa akikamatwa anazini, ilikuwa ni lazima auawe kwa kupigwa na mawe. Na hivi ndivyo sheria ilikuwa inataka iwe. Lakini utaona kwenye Agano Jipya, yule mwanamke mzinzi anapokamatwa na kuletwa mbele ya BWANA YESU, mwanamke yule anasamehewa na kuachiwa huru. Hii ndiyo "neema", yaani kwa neema tu anasamehewa ingawa Sheria inamuhukumu. Maana yake ni kwamba wale wasioipokea neema hii kwa kuacha dhambi zao, basi siku ya mwisho watahukumiwa kwa kutupwa kwenye moto kama Sheria inavyosema kuwa kila mzinzi, kama ni kufa na afe. Hivyo basi utaona "neema na rehema" zimepewa nafasi kipindi hichi ili watu wengi waokolewe, lakini wale watakaokataa kuzipokea rehema na neema hizi, hukumu ya moto inakuja juu yao.
MUNGU ni yule yule, MUNGU ni mkali sana, isipokuwa ni mvumilivu sana, tena anavumilia tu ili tuweze kujirudi na kuacha maovu yetu sababu hapendi hata mmoja wetu apotee. Hata yeye alisema kwa kinywa cha Nabii Isaya kuwa; "nimenyamaza kimya kwa muda mrefu, lakini sasa nitapiga kelele na kupaza sauti kama mwanamke aliye kwenye utungu wa kuzaa". Na kweli kabisa, sasa hivi MUNGU amenyamaza kimya, siyo kama zamani zile za Agano la Kale, lakini siku inakuja ambapo atapaza sauti yake, na hapo ndipo wanadamu na viumbe vyote watakapotambua hasira za MUNGU. Biblia inasema kuwa siku hiyo milima itakimbia na visiwa vitatoweka na mbingu zitafunguka kama vile mtu afunuavyo ukurasa wa kitabu. Siku ya ghadhabu na hasira ya BWANA MUNGU hakika inakuja.
Ndugu yangu RGforever MUNGU ni yule yule, jana, leo na kesho.