Je, Musa hakuandika kitabu cha Mwanzo??

jua,nyota na mwezi viliumbwa siku ya nne(kwa mujibu wa biblia)
siku tatu kabla mungu wako wa israeli alikuwa anaonaje wakati kulikuwa na giza?
Swali la kipuuzi sana hili, kwanza we unajua jua, nyota na mwezi vilikuwa wapi kabla ya kuumbwa??
 
Swali la kipuuzi sana hili, kwanza we unajua jua, nyota na mwezi vilikuwa wapi kabla ya kuumbwa??
sasa nani mpuuzi hapa!!!!!
niambie jua,nyota na mwezi vilikuwa wapi kabla havijaumbwa
 
Kikabwa naamini kilichoandikwa no matter nani kaandika
Shida ni kwamba kuna vitabu vimezuiwa kuwekwa kwenye bible kisa tu waandishi wake wana utata mfano kitabu cha Henoko au Injili ya Petro ama waraka wa paulo kwa wakaldea n.k huoni kuna double standards
 
Karibu sana mkuu Eiyer ni kitambo kidogo sijakuona jukwaani.....

Kwa ufahamu wangu uandishi wa vitabu vya Biblia umepewa na watu NJE YA BIBLIA ila kwenye biblia kuna vitabu vichache ndio vimeonyesha muandishi wa kitabu husika ni yupi??
Ahsante sana mkuu nishakaribia na naendelea kumshukuru Mungu kwa baraka na ulinzi wake kwetu....

Sasa mkuu kama sisi wasomaji ndio tunasema kuwa kitabu fulani kwenye biblia kimeandikwa na fulani na si kitabu chenyewe kinasema hivyo,sioni kama hata ni ishu ya maana kihivyo kwaababu msingi wake hauko kwenye maandiko yenyewe...

Jambo hili ninalifananisha na lile la kuhusu miaka ya dunia kwa wale wanaodai ni kwa mujibu wa biblia.Wengi wanadai umri wa dunia ni miaka 6,000 wakati biblia haijawahi kusema hivyo na ukiangalia muda huu kimsingi kwangu mimi naona si sahihi kabisa...

Jambo hili nalikataa kwasababu zaidi ya moja na hata mazingira naona kama hayarandani na jambo hili,nisiingie ndani sana kwenye hili kwasababu nalo ni mada kabisa,lakini ukweli ni kwamba suala hili na hili la nani kaandika kitabu gani nalo li yale yale tu...

Maoni ya watu yaendelee kuwa maoni ya watu na biblia iachwe kama ilivyo..
 
Nashukuru mkuu kwa clarification zako ila usiende mbali sana kuna mada controversial kidogo nimeandaa ila bado haijaachiwa nmekutag uje utoe darasa kidogo.
 
Dah!!


Hii biblia iliandikwa na ngumbaro haswa.

Fungakazi ni kwa hao waliovunjwa mapumbu yao tu kwamba wasimsogelee Yehova!

Hahahaaaaa!!
 
Musa kabla ya kufa,,Mungu alimwambia aweke mikono kwenye kichwa cha Joshua(naamini unamjua) kwa kumuwekea mikono alimuachia Joshua sehemu ya roho yake..Kwa hio muendelezo wa kuandika aliufanya Joshua ambae pia kwa kuwekewa mikono na musa nae Alikuwa nabii na kiongozi na yote aliokuwa akiyafanya musa.

Hili halileti kubatilisha chochote katika biblia ila kuvifanya vitabu vyote kuwa sahihi na visivyo na shaka yoyote.
Labda kuna vitabu vya kutilia shaka kama kitabu cha Enoch,,injili ya barnaba,,sijui injili ya eva,,injili ya mkapa na injili nyingine mpya mpya za kuanzia 1900s.
 
Mkuu zunguka kote duniani utafahamu Genesis imeandikwa takribani 500 BC ilihali musa alishakufa tokea 1400 BC sasa mbona hushangai Musa baada ya kufa miaka 800 imepita ndio mwanzo kinaandikwa ila unashangaa book of Enoch kuandikwa miaka mingi baada ya Enoch mwenyewe kufa???

Mimi nachopinga ni selective judgement Yaani unakataa Book of Enoch kisa kimeandikwa late ila hukikatai Wimbo ulio bora au waraka wa waebrania ambavyo mpaka leo waandishi wake hawajulikani??

Kwanini mkuu tunafanya hizi double standards??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…