Je, Muungano Bridge inawezekana Tanzania?

Je, Muungano Bridge inawezekana Tanzania?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
1634056667545.png

Taswira kwa hisani ya Google

Hii haiwezekani Tanzania? Kwanini isiwezekane? Nadhani hii ya juu tunaweza ila ya chini ya bahari ndiyo hatuwezi.
 
Nasikia wataalamu wa Japan walisema itatugharimu bajeti ya nchi ya miaka 20 kujenga daraja hilo! Faida zake ni nini labda.
 
Lina faida gani kiuchumi?
1. Miundombinu ya kurahisisha usafirishaji kwa bei nafuu kuliko anga na majini.
2. Kivutio cha utalii kwa Waafrika ambao ni 1.2 bl 16% ya watu wa dunia.
3. Mafunzo na utafiti kwa wataalam wa ndani na nje wakati wa kulimaintain.
4. Kuingiza fedha serikalini kupitia tozo za watumiaji.
5. Kuchochea ukuaji wa uchumi wa bluu.
6. Kuimarisha muungano wa Znz na Tanganyika. Moja ya vitu vilivyoimarisha muungano wa USSR ni ujenzi wa miundombinu ya reli ndefu duniani (9,288.2km) ya Trans Siberian Line toka Mashariki hadi Magharibi ya USSR (Moscow hadi Vladivostok) na kuifanya USSR kuwa Superpower duniani miongoni mwa sababu zingine kama gesi nyingi duniani, aina ya siasa na sayansi na teknolojia nk. Tz itakuwa Superpower EAC, GRL, Afrika SSH akijenga daraja hili kwa sababu itaendelea kupaisha nguvu ya kiuchumi ya Tz kwa kuwa na consumer market share/power kubwa kwenye kanda hizo kutokana na muungano ambao unafanya tuwe na idadi kubwa ya walaji.
7. Suez Canal ni ya pili kwa kuingizia Misri fedha mbali na Mapiramidi.

Badala ya kuwapa Wachina Bagamoyo tuwape hii wajenge kwa kanuni ile ya BOT (Build, Operate, Transfer) (Jenga, Endesha, Kabidhi serikali baada ya kurudisha mtaji na faida yako).

OIP.2eTzTG07ggNn6Nz8MUPElgHaE8

Trans-Siberian Railway Line.

maxresdefault.jpg

R.3010b0c90130e5fb774031506f47f0bf
 
Nasikia wataalamu wa Japan walisema itatugharimu bajeti ya nchi ya miaka 20 kujenga daraja hilo! Faida zake ni nini labda.
Mgodi mmoja tu unajenga Dar/Tanga-Pemba-Unguja. Tanzania tuna migodi inayofanyakazi na iliyolala zaidi ya 50.
 
Hamna tija yeyote hapo,

Kwan mizigo sasa hv haisafirishwi! Hela za kuwekeza kwenye project za hovyo kama hzi kwa nn zisitumikr kujenga viwanda vya kimkakati Tanzania! Hela ya kujenga hilo daraja itajenga viwanda vingapi Tanzania ambavyo vitakuwa na tija kubwa na kuinua uchumi wa Tanzania!!?

Sioni sababu ya kuendelea kuwekeza kwenye project zisizogusa maisha ya Watanzania! Unajivunia daraja refu then halina faida kwa nchi, ni uwekezaji wa kijinga!!
 
Mambo ya miundombinu aliyekuwa anaweza ni Magufuli peke yake, ndio katika kipindi chake cha miaka na nusu tumeona miradi mbalimbali ya miundombinu ikichipuka kama uyoga.
 
Hamna tija yeyote hapo,

Kwan mizigo sasa hv haisafirishwi! Hela za kuwekeza kwenye project za hovyo kama hzi kwa nn zisitumikr kujenga viwanda vya kimkakati Tanzania! Hela ya kujenga hilo daraja itajenga viwanda vingapi Tanzania ambavyo vitakuwa na tija kubwa na kuinua uchumi wa Tanzania!!?

Sioni sababu ya kuendelea kuwekeza kwenye project zisizogusa maisha ya Watanzania! Unajivunia daraja refu then halina faida kwa nchi, ni uwekezaji wa kijinga!!
Suez Canal inaiingizia Misri fedha lukuki sambamba na mapiramidi.
 
Ujenge daraja kufuata watu laki 8!!!? hu si uchizi?

Si Bora ukaenda kulijenga ziwa Tanganyika kwenda Congo?

kwenye popolulation ya watu milion 100+

Ndio maana nawaambia hi serikali haina washauri ni ujinga ujinga tu!!

Leo kwenda Congo tunapita Zambia wakati tunaweza Jenga daraja pale tena kwa ushirikiano tukawa tunailisha Congo bila kupitia Zambia na Burundi na Rwanda !!
 
Diaspora wameomba tuwape wajenge hili daraja.
 
Hamna tija yeyote hapo,

Kwan mizigo sasa hv haisafirishwi! Hela za kuwekeza kwenye project za hovyo kama hzi kwa nn zisitumikr kujenga viwanda vya kimkakati Tanzania! Hela ya kujenga hilo daraja itajenga viwanda vingapi Tanzania ambavyo vitakuwa na tija kubwa na kuinua uchumi wa Tanzania!!?

Sioni sababu ya kuendelea kuwekeza kwenye project zisizogusa maisha ya Watanzania! Unajivunia daraja refu then halina faida kwa nchi, ni uwekezaji wa kijinga!!
Basi angalikuwa magu hawaa......kusifia tu. Hapo mleta mada kaleta ndoto yake tu tayari mashambulizi utafikiri limetangazwa linatekelezwa
 
Back
Top Bottom