Je muuza miwa inawezakana kamuambukiza TB mdogo wangu?

ngungwangungwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
644
Reaction score
569
Mdogo wangu ambae ananisaidia kazi zangu,miezi miwili iliyopita aligundulika ana TB. Iligundulika baada ya kuwa na kikohozi kwa muda mrefu bila kupona. Alipoenda kupima kweli ikawa ni TB na sasa hali yake ni nzuri baada ya kuanza tiba! Hapa ofisini kuna jamaa alikuwa akimpitishia miwa maana mdogo wangu anapenda sana kula miwa.

Kila siku alikuwa akimpitishia kimfuko cha 200. Kilichotustua,yule jamaa aliacha kupita km miezi 3 hv. Leo kuna jamaa yake nae muuza miwa,tulimuita akatuuzia muwa wa 500. Wakati anamenya ndo dogo akamuuliza yule jamaa yuko wapi!? Kwa masikitiko akasema yule jamaa alifariki wiki 2 au 3 zilizopita na akazidi kueleza kwamba alikuwa anasumbuliwa na TB! Nimejaribu kuunganisha tukio hilo na ugonjwa wa mdogo wangu,hivi inawezekana alimuambukiza wakati anapuliza vile vimfuko kwa ajili ya kuweka miwa!!? Hebu wataalamu watuambie. Nawasilisha!
 
Mi naweza kuamin Ingawasi mtalaam,hao jamaa Pamoja na Wale wa karanga hua WanapuLiza kutanua mifUko.ni hatari
 
Mi naweza kuamin Ingawasi mtalaam,hao jamaa Pamoja na Wale wa karanga hua WanapuLiza kutanua mifUko.ni hatari
Mkuu,hata mimi nimefikiria sana juu ya tukio hili! Nadhani kuna haja ya kuchukua tahadhari kwenye biashara za aina hiyo.
 
Mi naweza kuamin Ingawasi mtalaam,hao jamaa Pamoja na Wale wa karanga hua WanapuLiza kutanua mifUko.ni hatari

Mkuu hiyo inawezekana kabisa, shukuruni kwa kupata matibabu mapema. hii imewahi kutokea zamani kidogo kupitia kwa muuza karanga.
 
Apime na Ukimwi kabisa hapo utagundua chanzo cha Tb ni nini.
 
Mkuu chakii, amepima hiyo hana!

Basi usihangaike kutafuta chanzo zaidi kwani uambukizaji wa TB ni rahisi sana hasa kupitia njia ya hewa hawa Mycobacterium Tuberculae ndipo wanapoishi.


Kikubwa azingatie lishe maana hizi dawa si mchezo.

Kila la kheri.
 
Last edited by a moderator:
100 percent inawezekana vimelea by tb husambaa kwa njia ya hewa kama muuza miwa alikuwa anapuliza vile vimfuko Lazima bacteria walipata nafasi ya kuspread coz hewa inayotoka mdomoni huwa ina mvuke
 
Hii kitu nilikua namuelezea jana rafiki yangu aache tabia ya kununua miwa ya kwenye vifuko maana anaweza kupata TB ..
Thanks na leo naona ushuhuda wa kitu nilichokuwa najaribu kumueleza jamaa

Si salama kula miwa ya njiani
 
We ukinywa dafu unaacha mate mule Halafu ule mti anaotolea nyama anautumia kwa madafu yote...so anahamisha TB from one to another
umekosea The boss hauwezi kupata TB kwa njia hiyo, TB(pulmonary tuberculosis) ni air-borne disease huambukizwa kwa njia ya hewa endapo mtu mwenye TB
atapiga chafya, miayo, kukoho etc nakutoa droplets zenye mycobacterium tuberculae na mtu mwingine akazivuta kwa pua na kuingiA kwenye respiratory tract na kuathiri mapafu hiyo ni pulmonary tuberculosis.
 
Thanks kwa info kuanzia leo sili miwa wala karanga za kwenye mifuko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…