ngungwangungwa
JF-Expert Member
- Jul 23, 2013
- 644
- 569
Mdogo wangu ambae ananisaidia kazi zangu,miezi miwili iliyopita aligundulika ana TB. Iligundulika baada ya kuwa na kikohozi kwa muda mrefu bila kupona. Alipoenda kupima kweli ikawa ni TB na sasa hali yake ni nzuri baada ya kuanza tiba! Hapa ofisini kuna jamaa alikuwa akimpitishia miwa maana mdogo wangu anapenda sana kula miwa.
Kila siku alikuwa akimpitishia kimfuko cha 200. Kilichotustua,yule jamaa aliacha kupita km miezi 3 hv. Leo kuna jamaa yake nae muuza miwa,tulimuita akatuuzia muwa wa 500. Wakati anamenya ndo dogo akamuuliza yule jamaa yuko wapi!? Kwa masikitiko akasema yule jamaa alifariki wiki 2 au 3 zilizopita na akazidi kueleza kwamba alikuwa anasumbuliwa na TB! Nimejaribu kuunganisha tukio hilo na ugonjwa wa mdogo wangu,hivi inawezekana alimuambukiza wakati anapuliza vile vimfuko kwa ajili ya kuweka miwa!!? Hebu wataalamu watuambie. Nawasilisha!