Wakuu
Nimekumbuka ile dhana ya muda mrefu kuwa mvua ikinyesha basi ni ishara kuwa simba anazaa huko porini. Je wewe ulisikia nini kuhusu jambo hilo? Na je uhalisia ni upi?
Nimekumbuka ile dhana ya muda mrefu kuwa mvua ikinyesha basi ni ishara kuwa simba anazaa huko porini. Je wewe ulisikia nini kuhusu jambo hilo? Na je uhalisia ni upi?
- Tunachokijua
- Watu wengi hususan kipindi cha utoto wao wamekuwa wakisikia kuhusu nadharia hii na hivyo kupelekea kurithishana vizazi hadi vizazi, kuwa mvu kunyesha wakati jua linawaka huwa ni dalili ya baadhi ya mambo ikiwemo Simba ama chui kuzaa ama fisi kuoa.
Mdau mmoja wa JamiiCheck.com aliandika kuwa,
Ni imani potofu. Nchini Rwanda, husema kwamba fisi anakuwa amevuta jiko.
Wadau wa JamiiCheck kupitia jukwaa la JamiiChec.com na mitandao yake ya kijamii wamethibitisha pia kuwa wameshawahai kusikia nadharia katika nyakati tofauti huku wengine wakieleza kuwa toka kipindi wanakua hadi leo wamekuwa wakisikia hivyo.
Mdau mmoja aliandika,
Toka nakua mpaka Leo naskia hivyo
Lakini Je, uhalisia ni upi?
JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa jambo hilo na kubaini ni la kisayansi huku hizo nyingine zikisalia kuwa nadharia na imani tu za watu kulingana na jamii husika kutokana na suala hilo kutokua la mara kwa mara katika maeneo mengi.
Jambo hili la mvua kunyesha wakati jua linawaka hujulikana kama Sunshowers ambapo inaelezwa kuwa mara nyingi hutokea wakati wa kiangazi na Masika. Hali hii husababishwa na sababu mbalimbali.
Miongoni mwa sababu zinazotajwa ni kuwa uwepo wa uwazi katika mawingu ya mvua na hivyo kuruhusu miale ya jua kupenya na kufika duniani kama kawaida wakati mvua ikiendelea kunyesha.
Sababu nyingine ni pale ambapo upepo husukuma matone ya mvua inayonyesha katika enelo lingine maili kadhaa kwenda katika eneo ambalo halina mawingu.
Makala inayopatikana katika tovuti ya WQAD inabainisha kuwa kisayansi zipo sababu mbili zinazopelekea kutokea kwa hali hiyo. Ambapo sababu hizo ni uwepo wa upepo mkali na sababu ya pili ni mawingu kutoweka haraka.
Matone ya mvua yanaweza kuchukua dakika kadhaa kufika ardhini baada ya kutoka kwenye wingu. Muda unaochukuliwa na tone la mvua kutoka angani hadi chini ni muhimu katika hali hii.