Gosbertgoodluck
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 2,855
- 402
Wakuu,
Kumekuwa na ubishani kati ya makundi mawili kuhusu mavazi wanayovaa wanawake. Kundi la kwanza linaunga mkono kwamba wanawake waachwe wavae kadri wanavyojisikia isipokuwa wanaume waache tamaa zao. Kundi la pili linasisitiza juu ya uvaaji wa heshima ili kuzuia tamaa za ngono kwa wanaume.
Kama wengi wetu tunavyofahamu, kuna uvaaji wa wanawake ambao umezidi kliwango kiasi kwamba hata anapopita mitaani, vijana wa kiume hupiga miluzi kuashiria jambo fulani. Swali langu ni je, mwanamke hata akiwa na umbo la kuvutia akivaa kwa heshima na kupita katikati ya vijana anaweza akapigiwa miluzi???
Mmh wanaovaa nusu wazi nao hawajafikia wengi kiasi chakuzoeleka????Ndugu
Mimi sitathubutu uvaaji wa nusu uchi hata siku moja, hata mtu aseme anaenda night club kujipumzisha nitamtofautishaje na malaya au changudoa???? Uvaaji wa nusu uchi sikubaliani nao hata kidogo, haijalishi unaenda wapi.
Nikirudi ktk point, uwezekano upo ila kwa sasa mi mdogo sana.
Ni mdogo kwa sababu hawa wanawake wenye maumbile ya kuvutia wapo wengi sana siku hizi, hivyo wamekuwa kitu cha kawaida kwa jamii ya sasa. Ila akivaa nusu uchi ndio miluzi itakuwa kama matarumbeta.
Na itakuwa ni haki yake
Mmh wanaovaa nusu wazi nao hawajafikia wengi kiasi chakuzoeleka????
Mkuu huoni kuwa haya mavazi ni ya utamaduni wa watu wa Afghanisatan?
Kivazi hiki poa kabisa....kutakuwa hakuna tatizo la kupiga miluzi au kelele za ajabu ajabu hata katika mitaa ya Kariakoo...Lizzy vipi unataka kutoa order yako?
Mkuu hakuna ubaya ila uvaaji huo dah! Mtihani.Naelewa sana Mkuu lakini sidhani kama kuna ubaya wowote kuyatumia katika mjadala huu.
BAK ninunulie basi na mimi ili wakwere wakose chakuangalia!
Navaa ili wale wasiotaka kuonyeshwa bila ridhaa yao waridhike!!hahahahaha lakini ulishaandika wengine wanakuvua nguo kwa macho kwa hiyo hata hii sijui kama itasaidia labda itapunguza kwa wale wasio na uwezo huo wa kuwavua Wanawake nguo kwa macho.
Huu ni mjadala mgumu kusema kweli maana Wanawake wengine hawakubali kabisa kuvaa mavazi yanayokubaliwa na wengi kama ni ya heshima. Kwa Mwanamke anaweza kabisa kuliona vazi lake ni la heshima lakini wengine wasione hivyo, sasa hapo ndiyo utata unapoanzia.
Uvaaji wenyewe ndio huu, alafu ukibakwa utasemaje?
Kivazi hiki poa kabisa....kutakuwa hakuna tatizo la kupiga miluzi au kelele za ajabu ajabu hata katika mitaa ya Kariakoo...Lizzy vipi unataka kutoa order yako? Maana kuna tetesi kwamba bunge litapitisha Sheria kwamba Wanawake wote wa Kitanzania (wenye umri wa miaka 15 kwenda juu) na Wageni nchini waanze kuvaa kivazi hiki ndani ya Tanzania kuanzia January 1, 2012 vinginevyo ni lupango ( hahahaha lol! I am just joking! 🙂 ) Imagine kwenda kucheza rhumba ukiwa umevaa hivi!?...kazi kweli kweli! LoL!