Je mwanaume mwenye tabia hizi anafaa kua mume?

kama issue ya hospital anaiongea kila siku yani hata wakitofautiana kidogo anaanza kumwambia kumbuka ulivokua unamwa nakupeleka hospital nani mwanaume gani angeacha mambo yake akusindikize hujui tu mwanaume kama mimi adimu, halafu watu wote wa maana anasema rafiki zake, mi mwenyewe ananiudhi sana anamasimango sana.
 
utafika muda fulani ataacha tu kwani hata hao anaowaambia mambo yake watamchoka.
 
utafika muda fulani ataacha tu kwani hata hao anaowaambia mambo yake watamchoka
 

hata kama anakuudhi ...huyo atabaki kuwa mpenzi wa rafikio mama! mpe ushauri ambao siyo biased then muache aamue mwenyewe! Chukua hizi thread ziweke kwenye pdf format ......print copy mbili zote mpatie yeye asomeeeee weee mpaka apate jibu. Akipenda anaweza akampatia jamaa yake copy nyingine asome ili ajue kumbe tabia yake inakera na ililetwa kenye bunge la wana-JF kujadiliwa.
 
thank you ntafanya hivyo ndo maana niliomba mawazo ya watu wengi, mimi mwenyewe kama rafiki yananitia hasira ndo maana niliona naweza kumpa jibu lisilo bora.
 
cjui kama Mamushka nimekupata vizuri, kwamba ishu ya huyu kaka ni macfa,hana la kuongea zaidi kujicfia...cjui kama nimekuelewa.


Issue ya huyu kaka hana siri na majisifa kila jambo lazima aliongee ,,inaboa sana
 
Mh hafai huyo jamaa, siku akikumega ukijamba tu basi mtaa mzima atasimulia karaha ya nini bibie mkimbie huyoo hahahahahahah
 

who cries?
 
looh rose hapo umechukua hatua kali mno, huyo inawezekana ni utoto tu akikua atatulia huyo amvumilie tu
hahah haah sawa bwana!!!!!!!
lakin kumbuka kuna tabia znazoendana na umri na kuna tabia ambazo ndo HULKA YA MTU..
anachokifanaya uyu bwana si tabia ya akikua ataacha ndo hulka yake ilivyoo...km katika kabila letu sisi kuanzia mtoto n'gaa kazaliwa leo mpk mbabu wa miaka wote ni mafagio kwwa kwenda mbele..yan ni kujisifia tu mpk ukikaa nao unajihisi wew u mpangaji apa dunian wao ndo wamiliki wa dunia na yote yaliyomo.......
 

..Rose, mi nilikuwa nasubiri ushauri wa nmna hii. Bado hamjaoana jamaa ni Bingwa wa kutangaza mambo yenu, mkiishaona si ndio atakuwa Champion kabisa na wewe huna la kufanya maana umeishajiingiza kwenye ndoa. Huyo binti anapaswa kumshukuru Mungu kwamba amemuonyesha kasoro hizi kabla hawajaoana. Huyo si wake. Atakapopata wake aliyepangiwa na Mungu hatamfuata rafiki yake kumuomba ushauri na rafiki yake akaja JF kutuomba ushauri...! Yeah, Amtoe balu.. Mwanaume hatakiwi kuwa na mdomo debe namna hiyo.

 

sasa anasubiri nin kumkimbiza?au ndo ivo ashaambiwa wanaume km yeye ni adimu sana?
kweli adimu ..wa sampuli iyo adimu tena adimu sana kuwapata.....(wa mafagio)
 

yaan ndg ayangu acha tu
uyu ata akinunua unga wa sembe ndan ni gumzo...kwenu hakuna ata unga..njaa tuu...dah mio siwez...ningemvumulia km hana ela lakin nisingemvumilia ata kwa dk 0 km mafagio+dharau zpo juu ivi..KWANINI UJISABMIT KWA MTU AMBAYE ANAKUONA WEWE NI TAMBALA ..kitunguu,kokroach...yaan sjui anakuonaje+na ayo matangazo yake km ya kampen dahh ningemkmbza na kishung cha moto km mwenge nakwambia..
 
sasa anasubiri nin kumkimbiza?au ndo ivo ashaambiwa wanaume km yeye ni adimu sana?
kweli adimu ..wa sampuli iyo adimu tena adimu sana kuwapata.....(wa mafagio)

hili fagio nadhani litakuwa lile la chelewa!!!!!!
 
jifunze kuandika kwa vituo, koma na paragraf... inatia uvivu kusoma

eish...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…