Dada,
Wanaochangia sana kuharibu mapenzi ya wapendanao ni watu wa nje. Chunga sana unapomshauri mwenzio kuhusu masuala ya mapenzi usiweke msimamo wako, jaribu ku-touch angles mbalimbali na mwisho wa siku mwache mwenyewe afanye maamuzi ya kunyoa au kusuka. Utakuja kuumbuka pale umemshauri aachane na huyo Domo Kaya wake then unawakuta wote pamoja wanafurahia malavi dave yao, siku hiyo utatamani ardhi ipasuke uingie wasikuone.
Ushauri wangu ni huu:
Kugundua source ya tatizo ni mwanzo mzuri wa kupata jawabu, sishauri akimbilie kwenye kuachana na jamaa kwani hizo tabia zinarekebishika. Kwa vile DomoKaya Wake amegundulika ni mtu wa kupenda misifa, basi mwana mama nae inatakiwa ampe complements za kutosha. Ikiwezekana amsifie vitu vya kijinga mpaka jamaa ajistukie kwamba mmmmh hapa kuna jambo mbona binti kabadilika.......taratibu jamaa ataanza kujirudi.
Anaweza pia kutumia marafiki wa huyo huyo mwanaume ( wenye busara lakini) kwa kuwauliza maswali kama vile; hivi ninyi mnaona rafiki yenu anafanya jambo jema kwa ku-expose mambo yetu ya ndani??? au Mbona jamaa huwa haji kunihadithia mambo mliyowafanyia wapenzi wenu?? yaani msg itamfikia tu huyo DomoKaya.
Asanteni!