Uchaguzi 2020 Je, Mwenyekiti Mbowe amemsusia Lissu kampeni?

Crimea

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
25,874
Reaction score
36,030
Mara ya Mwisho kumsikia Mbowe ni pale Mbagala alipowafokea TBC na kuwatimua mkutanoni siku ya uzinduzi wa kampeni za Chadema.

Sijamsikia tena toka hapo, ni kama vile ana kitu moyoni. Lisu anapambana peke yake huku na huko,.

Kampeni za mwaka huu Mbowe hana raha kabisa,! Hata jimboni kwake bado hajazindua kampeni mpaka leo.

Kuna mawili:

1. UKATA.
Juzi Membe kalalama kwamba wana hali mbaya kifedha huko upinzani, mapesa kutoka nje hayaingii selikali imezuia, marafiki wafanayabishara hawawachangii michango tena.
Kwa hoja hii ya Membe, Lisu anamkamua Mbowe kweli kweli, na kama mjuavyo Lisu ni masikini hana hela tofauti na Lowasa alitoa mabilioni yake pamoja na aliyochangiwa na friends of Lowasa yote yalijaa kwenye fuko la chadema ndio maana Kampeni za wakati ule kipindi kama hiki Mbowe alikuwa na furaha sana na alikuwa tayari ameshazunguka sehemu kubwa ya nchi wakiambatana na Lowasa.

2. AMEKATA TAMAA.
Yawezekana pia Mbowe kaona bora ajikalie kimya kuliko kuhangaika na kitu ambacho matokeo yake ni 0.
Yani wewe fikiria anaesikika ni Lisu peke yake, hata katika majimbo yote ni majimbo hayazidi 5 ambayo wapinzani wanaonesha uhai, kwingine kote ni kama hawapo. Hata lisu akifika kwenye mkutano anajinadi pekeake ni mara chache sana kusikia anawanadi wagombea wake wa ubunge na udiwani.

Kwenye huu uchaguzi Mbowe hajaingiza hata sh. 10 ila zinamtoka tu ndio maana kanuna sana.

Hebu ona furaha akiyokuwa nayo Mbowe enzi za EL kisha linganjsha na wakati huu
[emoji116][emoji116][emoji116]
 
Kampeni za mwaka huu ni tofauti na miaka iliyopita kila chama kina mikakati yake.
 
Lissu hahitaji kasaidiwa kama magu watanzania wote wanamkubali Mbowe anasuka mipango mingine subirini mtaona.
 
Mkuu kwanini Mbowe kanuna sana safari hii?
we unachekesha kweli, Mbowe pia ni mgombea ubunge kule Hai halafu unataka muda wote aambatane na mgombea urais kote nchini?!

itakuwa umetumwa na mbogamboga anayegombea Hai ili apate nafuu kwenye uchaguzi maana ni wazi atakuwa kabanwa kisawasawa
 
Lissu anawatosha wote, ukimwaga mboga anamwaga ugali, maji ya kunawa na kuivunja vunja meza ya chakula.

Lowassa alikuwa "muungwana" sana ilibidi nguvu ya ziada itumike kujibu kejeli na matusi kutoka upande wa pili.

Wanachofanya ni sawa na bora mwenyekiti na katibu washughulikie mambo ya nyuma ya pazia na mambo ya jukwaani wamwachie Lissu.
 
Tulieni tu mikakati ya CHADEMA safari hii hamtaiweza.
 
Nyie tatizo lenu mkiambiwa hamjitambui mnakataa mpaka sasa hivi angzunguka nae mngesema kalikimbia jimbo lake Lisu mwenyewe anawamudu endeleeni kupiga mayowe kama wafiwa mwenzenu Lissu anakimbiza kwa kutoa elimu ya Uraiya na kujitambu amkija shtuka mwana sii wenu Mungu aendele kuwapiga upofu hivyo hivyo

Sent from my BLL-L22 using JamiiForums mobile app
 
Sio kweli Mbowe muungwana Lisu alitapeli Chadema ili ateuliwe mgombea uraisi kwa ahadi kuwa Ulaya Kuna wafadhili kibao chini ya wakili wake Amsterdam ambao watatoa pesa za kampeni kwa wagombea wote Mbowe akampigia Na kumtumia email Amsterdam kuhusu Lisu alichosema Amsterdam akasema ni kweli kumbe fix kaona hela haiji na Lisu kaingiza Chadema madeni n.a. huyo tapeli wake Amsterdam hAkuna pesa zimetoka za kuwapa wabunge wala madiwani kwa ajili ya kampeni wao ndio wanahangaika kumwandalia mikutano Lisu badala ya yeye kuiandaa taarifa iliyopo kala pesa za wafadhii na kadeposit kwenye akaunti yake binafsi ubelgijia akusubiri uchaguzi uishe azitoe atokomee gizani sababu aligombea sio kwa Lengo la kushinda uchaguzi bali kuwapiga pesa wazungu wajinga wajinga sema Mbowe kashtuka ndio maana ka mute ila anamlia timing Lisu asijione mjanja ukiona Kobe kainama anatunga sheria akiinua kichwa Lisu kwa heri kisiasa
 
Ni kweli, nimempigia simu, ame confirm amesusa!
Kwa hiyo sisi humu tufanyaje? Maujinga tu.
Kutujazia uchafu humu daily!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…