Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
JE MWISHO UTAKAPOFIKA NITAKUWA NA CHAKUONYESHA? NISIJEGEUKA MCHAWI!
Anaandika Robert Heriel.
Hapo nilipomtembelea Babu yangu, Yule aliyenifundisha mambo mengi ya zamani na ya milele, ya Raha naya taabu! Ya gizani naya Nuruni, yote aliyojaliwa na Mungu kunifunza. Nikamtembelea siku zile, alikuwa amezeeka Sana, USO wake ulikuwa dhaifu Sana, macho yake yalikuwa hafifu Sana. Nilimuonea huruma mno. Nikamtazama ningali nakumbuka nasaha zake, hapo nikakumbuka nahau yake kuhusu ujani mkavu uangukapo kutoka mtini. Akanikumbatia!
Kisha akanong'ona sikuoni mwangu Kwa sauti dhaifu ya kizee; Taikon mjukuu wangu, huu ndio mwisho wangu, umeyaona Yale uliyojaliwa kutoka kwangu. Swali la mwisho nitakalokuachia mjukuu wangu ni hili! Je mwisho wako utaonyesha Jambo gani? Au nitageuka mchawi?"
Bado akaniachia!
Ndipo nikarudi mjini nikiwa na swali la Babu, swali lililozaa maswali mengi kichwani mwangu.
Kwa maana siku zakimbia Kama Farasi, zapaa Kama tai Kwa Kasi angani, nazo hazitupi nafasi tuziangalie zikija mbele yetu wala zikitupita hazituruhusu tuziangalie jinsi zilivyokwenda. Hizo ndizo nyakati na wakati, ambazo ukifikiri habari zake utapata wazimu.
Nitaonyesha nini Mimi jamani, mwenzangu Taikon najiuliza ni kipi nitaonyesha mwisho wangu utakapofika!
Mwisho wenye utisho, mwisho kilipo kifo, kabla sijakisalimia kifo naambiwa nitapaswa nikionyeshe mambo kadhaa ambayo niliyafanya Enzi zangu na wala hazikuwahi kuwa Enzi zangu kwani sikuwa na Enzi.
Je nitaonyesha Watoto pekee au nao watanikataa Kama Baba Yao?
Maana naambiwa wapo watoto hukataa wazazi wao hasa wakiwa fukara wakitaka kuwatoa kafara. Kipi nitaonyesha Mimi Mtibeli.
Je nitaonyesha mshamba au viwanja au majumba au magari, hayo yatajifariji kuwa nami nilikuwa na Enzi nilipokuwa napitia mapito yangu chini ya jua!? Kipi nitaonyesha ili ionekane Nina Enzi zangu nilipokuwa na nguvu!
Mwisho wangu nitaonyesha nini Mimi Taikon wa Fasihi, je ni falsafa zangu, maandiko yangu na vitabu vyangu nilivyokuwa naandika? Je hiyo ndio itaitwa Enzi zangu. Na vipi maandiko yangu yasiwe msaada Kwa kizazi hiko nitakapokuwa ninaufikia ukingo wa Nafsi yangu. Ole wangu Mimi ikiwa sitakuwa na Enzi ya maana wa kuuonyesha wakati utakapofika mwisho wangu.
Je ni hizi picha ninazopiga na kuzipost Mtandaoni ndio nitazionyesha mwisho wangu ukifika, zitamsaidia Nani hasa, au watoto na wajukuu zangu wataniona nilikuwa kijana Mpumbavu na zee jinga Sana. Watanishutumu na kunitusi kuwa Babu Yao nilikuwa mshamba wa Enzi ambaye nilikuwa mtumwa wa watu wengine. Doooh! Masikini Mimi!
Huo mwisho utakapofika bila hodi nitakuwa wapi?
Nitawaambia nini watu wa Enzi hizo, nitawaambia kuwa Maisha yalikuwa magumu? Lakini vipi wakiwepo rafiki zangu na ndugu zangu waliokuwa kama Mimi lakini wakawa na mambo ya kuonyesha?
Nitaonekana zee mjinga.
Unajua mwisho huwa ni maonyesho ya Yale uliyoyafanya katika mapito yako. Maonyesho ya Ukinho wa Nafsi. Je utakuwa na chakuonyesha?
Basi nikampigia simu Babu nikamuuliza yeye ilikuwaje! Akanijibu;
Kabla ya mwisho upo mwanzo, mwisho WA mwanzo ndio mwanzo WA mwisho.
Unapozaliwa Uhai ndipo kinapozaliwa kifo. Kifo na Uhai ni mapacha wasiofanana waliozaliwa siku moja kama usiku na mchana.
Akaendelea kusema; Uache kuzubaa Kwa maana Maisha yanazubaisha, ukiyaendekeza yanakusomba na kukutupa katika Mkondo mbaya wa majuto.
Usipokuwa na lolote la kuonyesha utageuka MCHAWI!
Babu yangu akasema alafu nikamsikia akikohoa, kohoo! Kohoo! Kisha simu ikakatika Mimi nikiwa bado naita Halo! Hallo!
Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa, wala sikutaka kuyafumbia macho mambo haya, nikasema nikushirikishe ewe ndugu yangu utakayepata ujumbe huu. Je mwisho utapofika utakuwa na chakuonyesha au ndio utageuka mchawi?
Tuzidi kupambana, tukimuomba Yule aliyemkuu!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kibaha