vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 2,474
- 4,726
Kuna tetesi kuwa Nabi ameamua kwenda kufundisha klabu ya Kaizer chief baada ya kufikiana makubaliano ya pande zote mbili.
Baada ya kuifundisha Yanga kwa misimu miwili yenye mafanikio kwa ngazi ya mashindano ya ndani na ya kimataifa, Nabi aliamua kutafuta changamoto nyingine huko Morocco na kushindwa kuifanya Far Rabat icheze hatua ya makundi klabu bingwa kwa kutolewa na Etoile du Sahel.
Nabi katika ligi kuu ya Morocco ameiongoza Far Rabat kwa michezo 29 na kushinda michezo 21, sare michezo 5 na kufungwa michezo 3 akiwa na point 68 nyuma ya Raja kwa point moja ikibakia mchezo mmoja kwenye ligi kuu.
Kama ligi ikiisha hivi, Nabi atakuwa ameshindwa kuifanya Rabati kutetea ubingwa wake aliopata msimu uliopata je ataweza kushindana na Mamelodi waliojitawalia ligi ya Afrika kusini au ndio anaenda kuua zaidi CV yake na kupotea kabisa?