jay-millions
JF-Expert Member
- Apr 30, 2015
- 3,983
- 10,034
Myika atawavusha wanachadema
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yeyote atakayegombea na kushinda.Kutokana na kupanda kwa joto la siasa nchi, hasa ukizingatia ujio wa chaguzi, mabadiliko ya Sheria ya uchaguzi na madai ya tume huru kutoka kwa wadau mbalimbali wa siasa.
Pia mfupa mgumu ambao umekuwa kama hadithi isiyo na mwisho. Maana mpaka sasa haijajulikana nani atakuwa na wajibu wa kumfunga paka kengele juu ya hitaji la katiba mpya ukizingatia mchakato unakwenda kwa mwendo wa konokono, huku hali ya kupoteza uaminifu kwa viongozi wa kisiasa ikipanda juu, kutokana na matukio kadhaa kutokea kwa pande zote mbili.
Mwisho upande mmoja tayari umesha toa la moyoni kupoteza imani ya mchakato wote.
Kwa sasa ni ukweli ulio wazi kwamba baadhi ya wanachama wa Chama Cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), wameanza kupoteza matumaini kwa kiongozi wao mkuu wa chama Mh. Mbowe jua ya siasa zake za kistaarabu ambazo chama Cha mapinduzi (CCM), kimetumia fursa hiyo kisiasa kuhujumu michakato ya mabadiliko mbalimbali ili kufanya usawa katika siasa kuwa mgumu na usio leta majawabu ya mkwamo wa kisiasa wa muda mrefu.
Baadhi ya matukio yaliyo sababisha Mh. Mbowe kuanza kutiliwa mashaka zaidi kulinganisha na lile la kumpokea Mh. Lowasa kwa sasa ni haya matatu.
Mosi, kitendo cha Mh. Mbowe kutoka gerezani kutokana na mashitaka ya ugaidi kufutwa na serikali kupitia DPP na kwenda moja kwa moja kuonana na mtesi wake Rais Samia Ikulu Dar es salaam.
Kitendo hiki kiliwakwaza sana baadhi ya wanachama wa CHADEMA na wadau wengine wataka mabadiliko ya kweli ya demokrasia ukizingatia Rais Samia tayali alisha onesha nia na dhamira ya kumfunga kupitia mahojiano na BBC.
Pili, Maridhiano Mh. Mbowe na Rais Samia pamoja waliasisi agenda ya Maridhiano kwa lengo la kuondoa mkwamo wa kisiasa ulio kuwepo nchi kipindi cha awamu ya tano chini ya Hayati Magufuli.
Matunda ya maridhiano yaleleta kufunguliwa kwa mikutano ya hadhara na baadhi ya watu waliokuwa na kesi za kisiasa kuachiwa huru, ruzuku nk. lakini jambo hili lilileta mpasuko ndani ya chama kwa maana kwamba ilitafsiriwa kama mbinu ya CCM ya kununua muda pia uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zao unalindwa na katiba sio matakwa ya mtu mfano wa wanachama walio tilia mashaka maridhiano ni Lema, Lissu nk.
Tatu, Agenda za maridhiano kufanywa siri, mambo mbalimbali yaliyo jadiliwa kwenye maridhiano yalifanywa siri, na hata pale alipo ulizwa kuhusu agenda muhimu hakutoa majibu yaliyo ridhisha, hivyo kufanya watu na wadau mbalimbali kuona jambo hili linafanywa kibinafsi zaidi na kupuuzia umma, ambao ndo walegwa na wadau wakuu na muhimu wa kutoa hamasa kwa serikali ili kutoa motisha kwa serikali kukubali matakwa kwa maslahi ya taifa.
Hivyo basi tayali imani ndani ya chama na wadau mbalimbali wa demokrasia imepotea juu ya Mh. Mbowe ambaye alikuwa karata muhimu ya kuleta mageuzi ya kisiasa nchini.
Ikitokea kama kukawa na shinikizo ndani ya chama kumtaka Mh. Mbowe ajiuzulu, naye akaona ni vema ili kukinusuru chama ili kuresha imani na motisha zaidi kwa umma.
Swali la msingi linaibuka hapa nani atafaa kuwa mrithi wa Mh. Mbowe kwa kipindi hiki kigumu cha mkwamo wa siasa nchini na kwenye chama na kwa sababu zipi mtu huyo anafaa kukalia kitu hicho muhimu.
Ukweli kafanya makubwa hilo liko wazi,lakini inabidi apumzike juhudi zake zitadumu kwa wana cdm.Nakumbuka Nyarandu aliwahi kugombea uenyekiti , na baada ya miezi michache akalamba ulabu wa ccm..
Kina upendo peneza walikuwa moto kuliko hata kina halima mdee na kina bulaya wakiwa viongozi wa bavicha na kanda lakini wote wamelamba ulabu wa ccm.
Hivyo Mbowe apewe maua yake, si kila anaye jua kuongea anaweza kuwa mwenyekiti wa chadema
Nashauri chadema wabadiri muundi wa uongozi ili kuwa na baraza la usalama la chama litakalo fuatilia nyendo za viongozi
UKWELI CCM imefanya makubwa sana, ila IPUMZIKE juhudi zake zitadumu tu hata kwa wana CCM!Ukweli kafanya makubwa hilo liko wazi,lakini inabidi apumzike juhudi zake zitadumu kwa wana cdm.