TFF wawe sirias, mpira unalipa kwa sasa. Watafute wawekezaji, wasiwe sehemu ya kukwamisha maendeleo ya mpira.
Logic ndogo tu! Miaka ya nyuma (2000 kurudi nyuma) timu za ligi kuu zilifika 20 kama sikosei, na wananchi walikuwa wachache tofauti na sasa.
Miundo mbinu ya usafiri haikuwa rafiki sana, na timu zilikuwa hadi zinalala njiani na mechi inahairishwa inachezwa siku nyingine, lakini timu zilipambana kumaliza mechi. Leo hii miundombinu ya usafiri imeimarika, sehemu yoyote ndani ya Tanzania hii ikiwa mbali sana unasafiri kwa bus na hazizidi siku mbili!
Kipindi hicho hela hazikuwepo nyingi kwenye mpira kama sasa, lakini wachezaji walijitolea sana miaka hiyo.
Leo, hamasa ya mpira imekuwa kubwa kila kona ya nchi, lakini TFF wanataka tuwe na timu 16, na baadae 14.
Leo, hela ipo kwenye mpira kupitia viingilio tofauti na zamani, lakini TFF wanataka kupunguza timu badala ya kuongeza timu.
Leo tupo watanzania milion 55-60, lakini TFF wanataka timu ziwe 16, kweli?
Afisa masoko wa TFF pambana, ligi yetu imechangamka kwa sasa, iuzeni ligi yetu mpate wadhamini.
Timu ziongezeke zifike 20. Mbona zamani iliwezekana?