Je, Nani anaweza kupata tiba ya Chiropractic?

Je, Nani anaweza kupata tiba ya Chiropractic?

Spinal Health

Member
Joined
Sep 19, 2023
Posts
12
Reaction score
10
Jibu la haraka ni mtu yoyote. Tiba ya chiropractic inasimama zaidi kwenye kinga kuliko tiba, unapata kinga kwaajili ya kuzuia magonjwa ya uti wa mgongo na magonjwa mengi ambatanishi. Ijapokua tiba hii watu wengi wanaitilia maanani wakiwa tayari wangonjwa amabo pengine hata kutembea hawawezi...lakini nataka kuwapa mtazamo mpya.
Tiba ya chiropractic ni kama kwenda hospitalini kwaajili ya kucheki afya ya meno yako (Dentist appointment) au kufanyia marekebisho gari yako baada ya muda fulani ( Car service) sio lazima gari iharibike ndo upeleke kwa fundi garage, lakini ukiweka tabia ya kwenda kwa fundi kila baada ya muda fulani, unazuia gharama kubwa ambazo zinaweza kutokea pindi gari yako imepata shida.
 
Back
Top Bottom