Je nani anaweza kuwashtaki Polisi walio muua Mwangosi

Je nani anaweza kuwashtaki Polisi walio muua Mwangosi

Mundungus Fletcher

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2009
Posts
327
Reaction score
79
Jana nilikuwa naangalia TV katika kubadilisha Badilisha station nikajikuta Mliman Tv. walikuwa na kipindi maalum kwa ajili ya David Mwangosi kwenye safari yake ya maisha. Wakawa wana wahoji waandishi waliokuwa kwenye tukio, hadi yule jamaa aliomgongea RPC kumuambia kwamba Polisi wako wanampiga mwandishi.
Katika hao wote waliohojiwq na kutoa ushuhuda, wote wali sema kwamba waliona kwa macho Polisi wakimpiga Mwangosi na hata yule askari alioshika ile bunduki. Na walidhibitisha kumuona RPC akishuhudia tukio bila kufanya lolote. Wamekuwa wakilalamika RPC ajiuzulu, Polisi watuhumiwa washtakiwe etc, mimi swali langu

Je kisheria, wahandishi wa habari hawawezi kuwashtaki Polisi walio kuwa pale na RPC wao?
Kwani ni lazima polisi wafikishwe mahakani na polisi wenzao? Meaning hakuna mtu mwengine au taasisi(LHRC, CHADEMA MCT nk nk) wanao weza kuwashtaki wale polisi ukiangalia ushahidi wote upo..?
Wataalamu wa sheria embu tusaidieni
 
Kabla ya kwenda huko tujiulize je? Kuna ugomvi gani kati ya polisi na vyama vya upinzani? Au kuna msukumo toka serikali?
 
.. mara nyingi uvunjwaji wa sheria, ukandamizaji,ukomoaji, visasi na mauaji yanayofanywa na kuwa na baraka na watawala. Maswali yake na utata wake ni mkubwa katika harakati za kutafuta haki na solutions!
 
Nchi za wenzetu hilo linawezekana, hapa kwetu kesi ya nyani huwezi kumpelekea ngedere
 
Back
Top Bottom