Je, Nape Nnauye anapaswa kushtakiwa kwa kauli aliyotoa huko Bukoba?

Je, Nape Nnauye anapaswa kushtakiwa kwa kauli aliyotoa huko Bukoba?

Kwa kauli hizi za akina Nape na wengine zinachochea hasira ya kiuchaguzi, tunahamasisha yaliyotokea Rwanda ya kimbari kama siyo leo kesho.Je tumeichoka amani. Tujirekebishe. na tuzikemee. vyombo vya dola fanyeni agenda ya kudumu bila kujali wadhifa wa mtu.
 
Kama kweli kaongea hii kauli, anatakisa kuwajibika au kuwajibishwa kujiuzuru.
Hapa anamaanisha tume ya uchaguzi haina kazi na pesa za uchaguzi zinaliwa bure na wajanja.
Na sisi wapigakura tunapoteza raslimali na muda wetu bure kukiamini Kiinimacho cha uchaguzi.
Kunyamaza ni njia nzuri ya kuficha upumbavu wa kichwani.
 
Kuna Video Ina Trend Mtandaoni ya Nape Nnauye akisema kwamba Yeye ni Mtaalamu na Mzoefu wa kuiba kura na kutangaza Matokeo ambayo sio halisi na kisha kuomba Msamaha kwa Mungu.

Lengo la Uzi huu ni kufahamu Je kauli hiyo kweli imetolewa na Nape?Je aliitoa Bukoba?Je Ni kauli sahihi kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Mawasiliano?

Pili Je kwa kutumia kauli yake tu hiyo Je anaweza kushtakiwa Katika Tume ya Maadili ya Utumishi wa UMMA au Hata Mahakamani kwa Kuvunja Sheria kwa kutumia kauli yake kama Ushahidi?

Tatu Je Rais wa Jamhuri ya Muungano analazimika kumuondoa Nape katika Nafasi yake ya Uwaziri kwa Kutumia Kigezo cha Kauli yake ili ambayo inaonekana ni ya kiuchonganshi hasa ukizingatia tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi mkuu?

Je Spika wa BUnge halazimika kumuita Nape kwenye Kamati ya Nidhamu na Hata kumfuta Ubunge kwa sababu ya Kauli yake Hii? Je, Tume ya Taifa ya Uchaguzi haipaswi kumshtaki Nape Nnauye kwa Kauli yake hii na Kumpiga Vita kushiriki katika Chaguzi zote za nchi na TUME kwa kutozingatia sheria na kanuni z Uchagui.

Nimeleta Uzi huu Hapa Fact Check Nikiomba Wataalamu Wa sheria,Katiba na Wafuatiliaji wa JF watafute Comments z Wote ambao nimewaweka hapa na wengine amba wanaweza kuwa na mamlaka na PIA NAPE NNAUYE ili kufahamu ukweli wa kauli na Msingi wa kisheria na kikatiba ambao unasimamia Viongozi wa Umma na MAwaziri.


Pia soma:Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Kauli ya "Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza" ilikuwa ni ya utani
Hatari demokrasia ya nchi yetu!
 
Back
Top Bottom