Salaam Wakuu.
Katika Hii dunia kila mtu anajambo/Mambo/kazi anayofurahia kufanya.Binafdi ninamambo kadhaa ila hiki nilichokifanya nimejikuta mimi mwenyewe najipiga kifua nasema Hapa nimefanya jambo kubwa linalostahili pongezi
Lakini, Je! Nastahili pongezi kwa hiki nilichokifanya?
Twende pamoja...
Binafsi ni Mdau mkubwa sana wa sekta hii adhwimu ya Technolojia niliejikita katika uwanja wa
Mobile & Web App Development kutengeneza Application mbalimbali za Simu,Tofuti n.k..Miezi kadhaa iliyopita nilipata tu fikra ambazo hata sijui zilipotokea. Nilipata wazo la kutengeneza Mobile App ya Vitabu Takatifu bila kubagua wala kuchagua dini.Yani App ya
Biblia Takatifu na
Qur-an Tukufu kadri nilivyozidi kutengeneza nilijikuta najawa Shahuku na Furaha sana Moyoni sijui ni kwanini?
View attachment 3127086
Muonekano wa App ya Biblia
View attachment 3127087 Muonekano wa App ya Qur-an
Amani na Furaha ziliendelea kutawala Moyoni Licha ya kwamba kila kazi haikosi changamoto basi moja ya changamoto kwenye Programming ni kupambana na Bugs na error za kutosha..Unaweza kukesha siku nzima unapambana na error ndogo kabisa ambayo badae unakuja kugundua baada ya kuchoka sana na kama unamoyo mdogo basi lazima ukate Tamaa.Binafsi hii haikuwa kikwazo kwani kila nilivyozidi kupiga hatua nilijikuta nadata zaidi niendelee mbele zaidi.
Hii Furaha ya ajabu ilitokea wapi?
Sina uhakika Furaha nayoipata ilitokea wapi, Lakini naweza kusema nimejifunza mambo mengi sana kwakuwa ni lazima upitie Kitabu kwa kitabu,Neno kwa neno au Aya kwa Ayah kuhakiki kama iko sawa au umeingia chakike..Kwahiyo kadri nilivyokua nasoma Neno/Surah kwenye App hizi nimejikuta navielewa sana na kubadili mambo baadhi kwenye fikra.
Licha ya hayo yote..
Kama zilivyo kazi nyingine basi kila kazi inaubunifu wake.Hivyo niliamua kuongeza manjonjo na makeke ili kuvutia zaidi watumiaji
Baadhi ya Feature zilizopo!!
View attachment 3127091
Katika hii Bible App kuna zaidi ya vitabu 1000 Na lugha kama zote zilizopo kwenye Uso huu wa dunia.Kwahiyo mtumiaji atatafuta Nchi yake na kujimwambafai humo ndani
View attachment 3127093
Mfano hapa kiswahili kipo kwahiyo ni raha tupu kwa msomaji
View attachment 3127094
Pia katika hii Qur-an tukufu kuna Juzuu zote 30 ,Surah zote 114 na Baadhi ya Tafsiri za Lugha mbalimbali ikiwemo kiswahili.
View attachment 3127095
Licha ya hayo.Pia utaweza kubadili mode Light/Dark theme kutokana na Muonekano anaopenda mtumiaji
View attachment 3127099
Vilevile utaweza kusikiliza audio za Neno au Qur-an surah yoyote na kwa Sauti mbalimbali
View attachment 3127101
Mambo ni mengi sana sana sana..Kuna kipengele cha Community ambapo hapa itakutanisha watu wa mataifa mbalimbali kuchat na kujadili Lakini hapa nitaweka jicho kama la Mods wa hapa JF kwakuwa Dini ni kitu sensitive kwahiyo hapakosi wapuuzi watakao kuja kuanza matusi, kejeli ,Dharau Nitawalamba sana
BAN .
Mwisho:
Binafsi nikiona watu au mtu hasa sisi ngozi nyeusi anambagua au kutukana mwenzie kisa tofauti ya kidini naona ni
MPUMBAVU na
MJINGA tu kwasababu hizi dini tumeletewa tu na hakuna aliekufa sababu ya kutokuamini..Russia,China,India ni mataifa makubwa na yenye maendeleo bila kuhusisha dini hizi mbili.
Nimalizie kwa kusema App hizi zipo kwenye hatua ya mwisho kwenye Playstore kwa watumiaji wa Android kama unataka kuwa Tester au wakwanza kuzipata basi nitaweka link kisha utanitumia email yako..Kwasasa nimeweka App ya
Qur-an Tukufu Playstore..Na kwa watumiaji wa iOS itachukua hata miaka kuiweka AppStore.
JE! Nastahili pongezi kwa haya niliyofanya?
Nawasilisha!