Je natimiza majukumu ya kuwa baba?

1menARMY

Member
Joined
Oct 5, 2011
Posts
17
Reaction score
1
Habar wanajf
mwenzenu nina tatizo naomben ushauri, nimeoa nina mtoto mmoja lkn mazingira ya kazi yangu magumu yanapelekea kuwa na familia yangu wiki mbili katika Miezi minne, je mnahisi natimiza majukumu ya famili kweli?ushauri tafadhari wapendwa?najiona sistahili kuwa baba!
 
Huo ni mwanzo wa kutojiamini ....................wasemeje wale walioenda kuhemea mbali kwa miaka 5? wao sio mababa?
 
Hizo mkuu ni imani yako tuu
Maana kama unatuimiza majukumu yako na familia yako inapata mahitaji yake huna haja ya kuwa na wasi wasi
Timiza majukumu ya kazi maana hata kwa hayo unapambana kuyaweka maisha ya familia mahali pazuri
 
Kama wewe hauna amani na unaona huitendei haki familia yako wakati uko huko mbali tafuta kazi ambayo itakuweka karibu na familia au mweleze mke wako atafute yeye karibu na wewe kwa mimi naona kama hiyo ya mbali inalipa na mnawasiliana vizuri sioni tatizo.pia weka malengo
 
Hakikisha familia inapata mahitaji yote muhimu unapokuwa mbali. Ukirudi home hakikisha mama anapata chakua chake inavyompasa na mwisho unapokuwa mbali hakikisha unawasiliana nao kila siku hii inasaidia kuonyesha unajali na kila kitu mpange pamoja haijalishi upo mbali. Hapo utakuwa unatimiza majukumu ya baba bila shida yoyote.
 
of course moja hapo hulitimizi kisawasawa,na wewe unalijua,mengine kama walivyosema wadau hapo juu so long as familia inatimiziwa mahitaji muhimu,hakuna tatizo.Simu muhimu kuwapigia kwa sana,ikiwezekana daily.Kuhemea muhimu ndugu yangu hata kama ni mbali.
 
ni jukumu moja tu ambalo hutimizi kwa mke wako, haki yake ya msingi
 
NI kweli kabisa maana kina mama wanasema mwanaume sio suruali wala kula sana, mwanaume ni pesa
 
maisha kutafuta,kama mkeo ni muelewa na mmekubaliana hamna tatizo!
 
Thanx wanajf hii kitu pasua sana kichwa yangu nashukuru kwa ushauri wenu wakuu
 
timiza majukumu yako kwa mkeo,mtoto na familia kwa ujumla.kama unafanya hvyo hakuna sababu ya kujiisi
 
Pole sana mkuu, jaribu kujiuliza haya maswali kwa muda!

1. je unaacha hela timilifu ya matumizi nyumbani na ya emergency?
2. Je huwa unapata muda wa kuongea na watoto na mkeo faragha?
3. Je unalipa karo ya shule ya watoto na kutoa kodi ya nyumba na bili za umeme?
4. Je huwa unawatoa watoto pamoja na mkeo out hata mara 2 au tatu kwa mwaka?
5. Je unampa mkeo unyumba hadi anarizika kwa huo muda unaokuwa nae karibu?
6. Je huwa unaijulia hali familia yako kila siku kama wamekula/wagonjwa/wanaendeleaje hapo nyumbani?
7. Je huwa unaongea na watoto kujua shida zao hata mara mbili kwa wiki ukiwa huko mbali?

Haya ni baadhi ya maswali ya kujiuliza kama mume/baba

Kama kuna mapungufu katika baadhi ya haya mambo, ichukue familia yako ili uishi nayo karibu na utimize majukumu yako yote!
 
ni hatari mno kumuacha mkeo kila mara alale peke yake...

lakini kwa kuwa wewe mwenyewe unajiuliza hilo swali
basi ni a good step
 
Kama unahakikisha kuwa mtoto anakula, anavaa, na kupata mahitaji mengine muhimu basi utakuwa umetimiza majukumu ya ubaba. Ila kuhusu majukumu ya mume, ambayo kimsingi hukuuliza hapa kwenye hii thread, nadhani majubu anayo huyo mamsap wako.
 
Hiyo nafasi ya wiki mbili ya kuwa nao pamoja kimwili uitumie vizuri.
Majukumu ya kazi hayakwepeki ila jitahidi kuwasiliana na familia yako mara kwa mara na kuisaidia inapokwama.
 
Watoto pia wanaitaji uwepo wa baba,hakikisha unawatimizia mahitaji yao lakini kumbuka kuongea nao kwa simu kujua maendeleo yao ya shule,homework na hobbies zao
Usijisahau ukawa uwasiliana na mama tu hapo watoto watakosa muongozo wa baba pia
 
Kwa maisha ya sasa hivi kuishi mbali na mkeo/mume ni hatari sana. Tumekuwa hatuaminiki hata tukiwa pamoja je kama hupo? nafikiri ni wakati mzuri wa kuangalia wapi ubase. Kama hilo swali limeshakuja kichwani mwako basi uwe mwangalifu na mengine mengi yanawezekana. Tafuta kazi karibu na mkeo ili uwe na amani.

Kazi zisiitufanye watumwa, weka mazingira mazuri ya wake zenu kujiajiri wenyewe. usikubali baba na mama kuamaka asubuhi wote mnaenda kazini. Weka miradi ambayo mkeo atasimamia hata siku umeacha kazi ghafla una pa kuanzia. Utakuta mke/mume asubui wangu wangu wanawahi kaziini. Mimi ilinilazimu niache kazi. Nimejiajiri nashukuru mungu naendelea vizuri.

Wale amba bado, hakikisha mna miradi mingi ya kufanya mama kukaa karibu na miradi iwe rahisi kuangalia familia kwa ukaribu. Ni hayo tu.
 

safi sana caroline, gud idea!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…