Je, naweza kubarikiwa kwa kutoa sadaka kubwa kubwa kanisani?

Je, naweza kubarikiwa kwa kutoa sadaka kubwa kubwa kanisani?

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Nimekulia kwenye familia ya KKIKRISTO made hebu ya Kilutheli, na Sunday School na Kipaimara nilikuwa mwanafunzi bora kabisa nikiwa nimekariri vifungu vingi sana vya Biblia.

Baada ya kuhitimu kidato cha sita, nilipata daraja la tatu, nikaona niingie mazima kwenye biashara maana hamna tena namna nyingine.

Kwa miaka mingi nilikuwa busy na kutafuta maisha na kanisani sikukanyaga kwa muda mrefu hadi pale nilipotaka kufunga ndoa.

Baada ya ndoa ndipo nikaanza kwenda kanisani, kulikuwa na ujenzi wa kanisa kubwa , nikaahidi mabati ya kutosha kuezeka kanisa zima.

Baadae nilikuwa kusakafia kwa malumalu kanisa zima. Sasa baada ya hapo nikajitolea kufunga vyoo vya kisasa kanisani.

Kumbe nimekaribisha tatizo, nimekuwa nikipigwa sana mizinga na wazee na viongozi wa kanisa. Huyu anataka ada, yule anataka kile, hadi sasa naona hata kero kwenda kanisani.

Leo mchungaji alinitembelea ofisini kwangu, tumeongea mengi sana. Mchungaji wetu ni mjanja na bado janki, hivyo tuna uwanja mpana sana wa kuongea.

Pia akaniuliza mbona mahudhurio yangu yametetereka Church, sikuona ubaya wa kumpa ukweli. Nikampa ukweli wangu kwamba mizinga na vibomu vimekuwa vingi.

Akaniambia nitoe tu kwa imani, Mungu atanibariki. Jamani kweli?
 
Screenshot_20230323-200633_WhatsApp.jpg
 
Wanakupiga tu hamna lolote! Saidia unapoona pana shida tena hasa wenye matatizo mahospitalini
 
Unajjla tu mjomba.Peleka kwa wahitaji live mbona wapo wengi mtaani hata maeneo yako ya biashara
 
Unabarikiwa zaidi ukitoa kile unachohitaji kwa kuishi na sio ziada ya kile ulichonacho.

Itakua uli doji hili somo kipindi cha Sunday school [emoji538]
 
Kwanza Sadaka kubwa ni ipi?

Sadaka sio Ukubwa wa kitu au wingi wa fedha, Mungu anaangalia moyo na Utayari wako wa kumtolea

Naweza kutoa elfu 2 mwingine akatoa Mil.10 katika ibada moja lakini sadaka yangu ikapata kibali mbele za Mungu, wa Mil.10 atapata kibali na sifa kemkem kwa Wanadamu

Kutoa sadaka ni Moyo sio Uwingi.
 
Back
Top Bottom