Je, naweza kumshitaki Boss wangu kwa hili?

Je, naweza kumshitaki Boss wangu kwa hili?

Rutorial k

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2014
Posts
960
Reaction score
855
Hello wanasheria! ni matumaini yangu mko salama.

Nahitaji msaada wa kisheria kuhusu hili. Mimi ni mwajiriwa katika sekta binafsi. Yani ni mwalimu katika shule ya sekondari katika mkoa fulani. Ninao mkataba wa mwaka mmoja ambao utaisha mwaka huu Desemba.

Hoja kuu ni kwamba kutokana na ugonjwa wa CORONA bosi wangu ni kama amenitelekeza (ametutelekeza)....mwisho wa mwezi umepita hakuna mshahara wala taarifa yoyote kuwa atatoa mshahara lini. Kibaya zaidi mwisho wa mwezi watatu tulienda ofisini kama alivyotuahidi ili kupokea chochote hakutujali kabisa. Hakutuambia chochote zaidi ya kupanda gari lake na kuondoka na kutuacha tumekaa kwenye mabenki.

Kwa hiyo wajuvi wa mambo ya kisheria napenda kujua kama naweza kumshitaki bosi wangu, nifungulie mashitaka gani huyu bosi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom