wanajamvi nilipata ajali ya jicho utotoni nilichomwa na katani jichoni,nilikimbizwa hospitali ya Nkinga nikapata operation pale lakin baada ya hapo jicho langu lilikaa upande na hivi sasa ninaonekana kama nina makengeza!So nikua na nina miaka ishirini na nne nataka kama kunauwezekano nifanyiwe oparation tena!Je naweza kufanyiwa operation na jicho likakaa sawa??na niende hospital gani??
Nenda CCRBT, Dar es salaam, kuna specialists wa macho wengi, usikatishwe tamaa na wajinga wachache wanaokujibu kwa kukutanisha tamaa
wewe jikubali tu usije kosa kengeza ukapata chongo.....
Ni bora ukamwona specialist wa macho akukupe jibu mwafaka.
Km jicho lako halina shida ungebaki hivyohivyo ndugu au una ona haya kwa kuwa kengeza
Pole km halina shida acha tu,ila samahanini wanajamvi kuna tiba ya macho kwa njia mionzi kuna yeyote mwenye hufaham wa hii tiba?
Haya km umeamua lkn km hakuna ulazima bora ungeliacha ,maana usingetengeneza ugonjwa mwingine
pole sana, pale Regence Hospital kuna Specialist mzuri wa macho,.
Jaribu kwenda utapata msaada wa tatizo lako!!!