G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Gubu ni neno la kiswahili ambalo tafsiri yake ni mtu kuwa na hasira na kupaniki hovyo hata kwa jambo ambalo ni la kawaida. Mtu huyo mara nyingi ni mgomvi mgomvi, mlalamishi, anayenuna nuna hasa pale anapoelekezwa jambo, kuadhibiwa kwa kosa lake au kuonywa! Hivyo gubu siyo tusi.
Sasa basi kutokana na "trend" ya maugomvi, visa, watu hasa vijana wadogo kuwekwa mahabusu kwa vijikesi vya ajabu ajabu, ugomvi na majirani kwa vitu ambavyo mkikaa chini mnavimaliza! Je, wapo watu au mtu ambaye ana nguvu ndani ya mfumo mwenye gubu?
Chukulia mfano huko Singida vijana wadogo wa CHADEMA wamekamatwa ila kila siku ya kesi yao wao lazima kitoke kisingizio ooh mara hivi mara vile yani ilimradi kuwakomoa tu na zaidi ya wiki mbili sasa wapo mahabusu. Kosa lenyewe eti walipandisha bendera ya CHADEMA huku wakiimba wimbo wa taifa. Haki ya mtume wallah!
Mfano mwingine ni sakata la ujirani na Kenya. Wao Kenya walitoa tangazo lao la kwanza kuwa wataruhusu watu wa mataifa 11 kwa hatua ya awali kuingia nchini humo. Yamo mataifa mengi tuu ikiwemo Marekani wamepigwa pin kuingia humo na wameheshimu kwakuwa wanajua maana yake! Ila sisi sasa, yani hata masaa12 hayajafika tayari tunarusha mijiwe "full" mvurugano bila tungamo. Ona walivyorudi na staili nyingine tunaonekana ni watu tusio na uvumilivu, wala majadiliano "Yaani GUBU"
Mtu akikosoa kidogo tu tena kwa mambo yenye uhalisia kinachofuata ni adhabu! Ukiwa mfanyakazi au mfanyabiashara halafu uwe against CCM "ADHABU" Hii kama siyo "GUBU" ndani ya huu utawala wa awamu ya tano ni nini? Ukiongea ukweli mchungu kwa serikali adhabu na tena utakuwa unaandamwa kila siku!
Narudia tena, Gubu siyo tusi bali ni neno linaloelezea tabia ya mtu kuwa na visasi vibaya na mlalamishi!