Je, Ndege inawezaje kupaa angani?

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Ufafanuzi Mdogo

Kumbuka ndege ina viungo vya msingi vinne (PrimaryComponents) 🛩

1. Bodi/Kiwiliwili (Fuselage) kubeba abiria au mizigo.
2. Mbawa (Wings) kupaisha ndege na kubeba mafuta.
3. Mkia (Tail) kushikilia uelekeo wa ndege.
4. Injini: kusukuma ndege (Thrust)

Kila ndege ina mwendo wake ambao ikifika mbawa zinatengeneza "pressure" ya kutosha kuweza kunyanyua (Lift Off)

Ndege inapokimbia katika njia ya kuruka (Runway) hewa inayokuja kutoka mbele inagawanywa mara mbili katika mbawa ambapo moja hupita juu na nyengine chini.

Kutokana na umbile la mbele ya mbawa (leading edge) hewa inayopita juu ya mbawa inapita kwa kasi zaidi kuliko hewa inayopita chini.

Hali hiyo inapelekea hewa inayopita chini ya mbawa kuwa na mkandamizo mkubwa (HighPressure) kuliko ipitayo juu ya mbawa kadri ndege inavyoongeza kasi.

Hewa yenye "pressure" kubwa chini husukuma mbawa juu na ndege kuanza kunyanyuka taratibu (Lift)
Lakini ili iweze kunyanyua mbele na kupaa rasmi turudi kwenye vidhibiti vya mkia (TailControlSurface)

Mkia una mbawa ndogo mbili zilizolala (Horizontal stabilizer) zenye vidhibiti viitwavyo "Elevator".

Mkia uliosimama (vertical stabilizer) una kidhibiti kiitwacho "rudder".

Vidhibiti vya mkia uliolala kazi yake kuelekeza pua ya ndege kwenda juu au chini (Pitch) kulingana na maamrisho ya Rubani.

Endapo vidhibiti hivyo (elevators) vikigeuzwa na Rubani kuangalia juu pale ndege ikifikia kasi inayohitajika itaanza kunyanyuka mbele na kupaa kwasababu hewa inayopita mkiani itakinzwa upande wa juu na kukandamiza mkia kwenda chini hivyo kupelekea ndege kunyanyuka mbele.

Hali kadhalika na kinyume chake kama ndege ikiwa angani na rubani anataka kuanza kutua vidhibiti hivyo vitageuka kuangalia chini ambapo hewa inayopita chini ya mkia itakinzwa na kusukuma mkia juu ambapo upande wa mbele utalazimika kupelekea chini.
(Hii inafanya kazi kama mzani)

Na kidhibiti cha mkia uliosimama (Rudder) pia kazi yake kuelekeza pua ya ndege kwenda kulia au kushoto (Yaw).

Endapo kidhibiti hicho (rudder) kitageuka kulia basi hewa ya upande huo itakinzwa na kusukuma mkia kwenda kushoto hivyo pua ya ndege italazimishwa kwenda kulia na kinyume chake.

Kwahiyo wakati ndege imefikia kasi yake ambayo hewa ina 'pressure' ya kutosha kuweza kunyanyua mbawa Rubani anaamuru vielekezi vya mkia uliolala (Elevator) kugeukia juu ambapo vitakinzana na hewa ipitayo juu kuweka uzito na kulazimisha mkia kwenda chini na pua kuelekea juu na kupaa.

Mbali ya yote, ndege huwa na vifaa vingine vinavyosaidia ndege kupaa na kutua kwa urahisi pasipo kuhitaji kasi kubwa sana.

Vifaa hivyo (lifting devices) vinavyochomoka na kuinama nyuma ya mbawa huitwa "flaps". Ndege za kisasa zina vifaa vingine vya ziada kama 'Slats' mbele ya mbawa, Trims kwenye vidhibiti vya mkia n.k

Lakini pia Kuna 'Ailerons' kila bawa kwaajili ya ndege kulala kushoto au kulia hasa inapohitaji kukata kona angani kwa kusaidiana na kidhibiti cha mkia "rudder". Pia husaidia kuweka ndege sawa pale inapoyumba (Aerodynamic Steering)

(Kumbuka ufafanuzi huu haikufanyi kuwa Rubani 👮)
 
Duh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…