KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
- Thread starter
- #21
TrueLkn pia ufafanuzi huu hukufanyi uweze kutengeneza ndege
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
TrueLkn pia ufafanuzi huu hukufanyi uweze kutengeneza ndege
Hizi ni hints tu za kukufanya upate mwanga kidogo tu
Comment hii ipewe maua yakeUtani tu huo, si ajabu hata baiskeli hajui kuendesha sembuse ndege 🤣
Hicho kinachofanya pressure ya hewa iwe ndogo juu na iwe kubwa chini ya bawa la ndege ndio msingi mkubwa wa kupaa kwa ndege mengineyo ni just decorations, thanks to Bernoulli the pioneer of the principle and its mathematical formulation.
Comment hii ipewe maua yake
Asante sanaJust humbled 🙏🏻🙏🏻, na wewe pia upewe maua kwa kutupatia elimu nzuri.
Mbuzi kazi yake kuliwa, hata akifia chumbani ataliwa, na mtasema mbuzi kagoma kwendaTutapambana tu lazima mbuzi afie Kwa muuza supu
Appreciation to you tajiri mkuu wa matajiri. [emoji122]Ufafanuzi Mdogo
Kumbuka ndege ina viungo vya msingi vinne (PrimaryComponents) [emoji927]
1. Bodi/Kiwiliwili (Fuselage) kubeba abiria au mizigo.
2. Mbawa (Wings) kupaisha ndege na kubeba mafuta.
3. Mkia (Tail) kushikilia uelekeo wa ndege.
4. Injini: kusukuma ndege (Thrust)
Kila ndege ina mwendo wake ambao ikifika mbawa zinatengeneza "pressure" ya kutosha kuweza kunyanyua (Lift Off)
Ndege inapokimbia katika njia ya kuruka (Runway) hewa inayokuja kutoka mbele inagawanywa mara mbili katika mbawa ambapo moja hupita juu na nyengine chini.
Kutokana na umbile la mbele ya mbawa (leading edge) hewa inayopita juu ya mbawa inapita kwa kasi zaidi kuliko hewa inayopita chini.
Hali hiyo inapelekea hewa inayopita chini ya mbawa kuwa na mkandamizo mkubwa (HighPressure) kuliko ipitayo juu ya mbawa kadri ndege inavyoongeza kasi.
Hewa yenye "pressure" kubwa chini husukuma mbawa juu na ndege kuanza kunyanyuka taratibu (Lift)
Lakini ili iweze kunyanyua mbele na kupaa rasmi turudi kwenye vidhibiti vya mkia (TailControlSurface)
Mkia una mbawa ndogo mbili zilizolala (Horizontal stabilizer) zenye vidhibiti viitwavyo "Elevator".
Mkia uliosimama (vertical stabilizer) una kidhibiti kiitwacho "rudder".
Vidhibiti vya mkia uliolala kazi yake kuelekeza pua ya ndege kwenda juu au chini (Pitch) kulingana na maamrisho ya Rubani.
Endapo vidhibiti hivyo (elevators) vikigeuzwa na Rubani kuangalia juu pale ndege ikifikia kasi inayohitajika itaanza kunyanyuka mbele na kupaa kwasababu hewa inayopita mkiani itakinzwa upande wa juu na kukandamiza mkia kwenda chini hivyo kupelekea ndege kunyanyuka mbele.
Hali kadhalika na kinyume chake kama ndege ikiwa angani na rubani anataka kuanza kutua vidhibiti hivyo vitageuka kuangalia chini ambapo hewa inayopita chini ya mkia itakinzwa na kusukuma mkia juu ambapo upande wa mbele utalazimika kupelekea chini.
(Hii inafanya kazi kama mzani)
Na kidhibiti cha mkia uliosimama (Rudder) pia kazi yake kuelekeza pua ya ndege kwenda kulia au kushoto (Yaw).
Endapo kidhibiti hicho (rudder) kitageuka kulia basi hewa ya upande huo itakinzwa na kusukuma mkia kwenda kushoto hivyo pua ya ndege italazimishwa kwenda kulia na kinyume chake.
Kwahiyo wakati ndege imefikia kasi yake ambayo hewa ina 'pressure' ya kutosha kuweza kunyanyua mbawa Rubani anaamuru vielekezi vya mkia uliolala (Elevator) kugeukia juu ambapo vitakinzana na hewa ipitayo juu kuweka uzito na kulazimisha mkia kwenda chini na pua kuelekea juu na kupaa.
Mbali ya yote, ndege huwa na vifaa vingine vinavyosaidia ndege kupaa na kutua kwa urahisi pasipo kuhitaji kasi kubwa sana.
Vifaa hivyo (lifting devices) vinavyochomoka na kuinama nyuma ya mbawa huitwa "flaps". Ndege za kisasa zina vifaa vingine vya ziada kama 'Slats' mbele ya mbawa, Trims kwenye vidhibiti vya mkia n.k
Lakini pia Kuna 'Ailerons' kila bawa kwaajili ya ndege kulala kushoto au kulia hasa inapohitaji kukata kona angani kwa kusaidiana na kidhibiti cha mkia "rudder". Pia husaidia kuweka ndege sawa pale inapoyumba (Aerodynamic Steering)
(Kumbuka ufafanuzi huu haikufanyi kuwa Rubani [emoji61])