kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Wandugu kuna ile ndege ya shirika letu la ndege ATCL iliyoshikwa je, imeachiwa au ndio tena basi?
Inaonekana hakuna uwazi huku ikielekea kuna shinikizo toka nje kwamba nchi iangalie upya miradi iliyoanzishwa chini ya JPM kutokana na ilani za CCM.
Kuna hofu kwamba kuna wajanja au wahuni wanaotaka kuhujumu nchi kwa kisingizio ndege kukamatwa na mtu mwenye kuidai nchi huku akisaidiwa na vigogo wahuni kuiuza ndege na genge hilo kugawana hela.
Ni muda sasa tangu kisa cha kukamatwa ndege ya ATCL katika mazingira hayajawekwa wazi.
Umma wa wananchi wangependa kujua ni ndege gani ilikamatwa na imekamatwa wapi, na kama ilienda hapo kwa shughuli gani hadi ikakamatwa?
Je, ni hizi ndege mpya zilizonunuliwa kwa fedha taslimu kuanzia awamu ya tano au ni nyingine? Pia wananchi wangetaka kujua kisa hicho kiko hatua gani na hatua gani imefikiwa kutatua, na kama ndege ni kweli imeuzwa kama wengine wanavyodai?