Baada ya kukutana na taarifa kuwa majeshi ya majini ya Iran yameshambuliwa nimeenda dip ili kujua chanzo cha sababu hiyo ila chaajabu ni kwamba nimekutana na taarifa tofauti je nikweli ilikuwa mashambulizi au taarifa zimechanaganyika?
- Tunachokijua
- Iran ni nchi iliyopo Mashariki ya kati, upande wa Ghuba ya Uajemi (Persian Gulf). Ni nchi yenye rasilimali kubwa za mafuta na gesi, na ina nafasi muhimu sana katika siasa za Mashariki ya kati na ipo upande wa kaskazini katika mlango wa Hormuz.
Madai
kumekuwepo na taarifa iliyoambatana na picha zinazosambaa mtandaoni inayodai kuwa ndege za kivita za B-2 spirit zimeteketeza jeshi la majini la Iran katika mlango wa Hormuz na ikidai kuwa tukio hilo limetokea 10 August 2026
Uhalisia
Baada ya ufuatiliaji wa kidigitali imebainika kuwa taarifa hiyo si ya kweli. Hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha mashambulizi hayo kwa siku ya Agosti 10, 2026.
Ufuatiliaji zaidi kwa kutumia reverse image search umeabaini kuwa picha iliyotumika kwenye taarifa hiyo imekuwepo mtandaoni kuanzia Februari 25, 2015 ambapo vyanzo vilikua vikiripoti kuwa hayo ni mashambulizi ya Iran kwenda kwa Marekani na si kama taarifa potoshi inavyoeleza. Tazama vyanzo hivyo hapa, hapa na hapa.