Je, ni Biashara gani inaendelea hapa?

Je, ni Biashara gani inaendelea hapa?

Heisenberg

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2017
Posts
1,691
Reaction score
2,967
Kwa wale ambao huwa mnapita maeneo ya magereji kama vile Tandale, Mwananyamala, Ilala na Kko bila shaka umeshawahi kuwaona watu wakipita na baiskeli au mikokoteni wakikusanya Madumu/ Chupa za oil za magari na pia wakikusanya oil chafu na kuondoka nayo.

Baada ya utafiti kidogo inasemekana oil hiyo inatumika kama fuel kuendesha mitambo inayotumia mafuta mazito, na wengine wanasema Oil hiyo hufanyiwa Recycling na kurudishwa kwenye matumizi. Na kuhusu Vidumu hasa hivyo vya kuanzia Lita 4 na kuendelea huwekwa oil Isiyo ya brand husika na kurudiashwa kwenye soko

Je! Umeshawahi kukutana na hali hiyo?
IMG_1715.jpeg
IMG_1731.jpeg
IMG_1721.jpeg
 
Huu mji hakuna linaloshindikana inawezekana baadhi ya engine oil Fulani zinatokana na oil chafu...hii yote inatokana na Sisi watanzania kupenda vitu vya bei cheee
 
Hii oil sio salama kwa matumizi y engine yoyote ile…
Ilipaswa matumizi yake kuelekezwa kwny uuaji wa mazalia y mbu, kupakwa kwny mbao za kuezekea kuzuia wadudu.

Kutumika kwny viwanda vya chuma kuyayushia vyuma na majiko au vitu km hivyo…

Oil isio na brand haifai hata kwa engine y tractor….. cheap is expensive
 
Wengi tunakutana nao sema hatujawahi kujiuliza tu au tunapuuzia.

Nishawahi sikia pia inachukuliwa inaenda katika viwanda vya kuyeyusha vyuma na inatumika kupoozea mashine.

Ila nishawahi sikia pia Kariakoo kuna watu wanazisafisha kisha wanapark
Kwenye madumu ata yenye brand kubwa kisha wanauza, hii inawahusu wazee wa “fundi njoo chukua gari kanifanyie service” mwenzio anaenda anaweka oil ya elfu 7 lita moja.
 
Kwa wale ambao huwa mnapita maeneo ya magereji kama vile Tandale, Mwananyamala, Ilala na Kko bila shaka umeshawahi kuwaona watu wakipita na baiskeli au mikokoteni wakikusanya Madumu/ Chupa za oil za magari na pia wakikusanya oil chafu na kuondoka nayo.

Baada ya utafiti kidogo inasemekana oil hiyo inatumika kama fuel kuendesha mitambo inayotumia mafuta mazito, na wengine wanasema Oil hiyo hufanyiwa Recycling na kurudishwa kwenye matumizi. Na kuhusu Vidumu hasa hivyo vya kuanzia Lita 4 na kuendelea huwekwa oil Isiyo ya brand husika na kurudiashwa kwenye soko

Je! Umeshawahi kukutana na hali hiyo?
View attachment 3036727View attachment 3036728View attachment 3036732
Oil chafu ina matumizi mengi
Dawa ya kuulia wadudu
Kuwa recycled na kutengeneza mafuta yanayojulikana kama IDO (Industrial Diesel Oil)
Nishati kwa ajili ya kuchemshia lami kwenye site nknk
Hiyo ni biashara kubwa yenye faida nono ila usiingie kichwakichwa unaweza kupigwa
Aina za oil chafu
Engine oil (the best)
Hydraulic oil
Sladge toka kwenye meli na matank makubwa ya kuhifadhia mafuta
 
Back
Top Bottom