Mkuu International Business ni biashara ngumu sana inayo hitaji kujipanga sana, ni tofauti sana na Domestic trade,
Kwa upande wa Bidhaa za ku export nje ziko nyingi sana ila kuna matatizo kadha wa kadha kama ifuatavyo
1. Quality- Mkuu kuingiza bidhaa Ulaya au Marekani si kitu cha mchezo kabisa hasa vyakula na ndo maana Ulaya na marekani tunauza Vinyago pamoja na Pamba, hii ni kutokana na sheria kari sana za maswala ya Ubora ili kuwalinda wananchi wao
- Kwenye swala la matunda kuna soko huko but kumeet quality standard yao ndo kazi pevu sana
2. Quantity- Mkuu quantity nayo niatatizo kubwa sana, kunawatu wengi wamepata masoko lakini kwenye quantity imekuwa kazi sana,kuna jamaa yangu alipata soko la mafuta ya alzeti lakini alishindwa kwa sababy ya qiantity, wanaweza kuambia wanataka tani laki 5 za mafuta ambayo hayajasafishwa ya alizeti, utazitoa wapi
- Mara nyingi qunatity nayo ni kikwazo kikubwa sana make wanataka in volume so inawawia vigumu kusaply
3. Competition- Tambua kwamba ukipata soko mfano la Matunda huko ulaya unakwenda kushindana na nchi za ASIA ambazo zinasifika kwa kulima matunda sana na mbogamboga, au unashindana na wakulima wa huko huko ulaya na asia
4. Vikwazo vya kibiashara- Kuna vikwazo vingi sana kwa upande wa kibiashara, mfano Jumuia ya ulaya wao wanalinda wazalishaji wao so wanaweka sheria kari sana na kodi kubwa kwa wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya jumuia ya ulaya. marekani nayo ni hivyo hivyo,
-Ila Wanachama wa Jumuia ya ulaya wao wanauza bila shida ndani ya jumuia yao ni kama ilivvo kwa East Africa comunity
5. Ghalama za uzalishaji - Ghalama za uzalishaji huku Bongo ziko juu mno kiasi kwamba inakuwa vigumu ku export na still umeki profit,
- Kuhusu masoko, mkuu mara nyingi masoko unatakiwa utafute mwenyewe na usitegemee serikari ndo ikutafutie masoko na,
MASOKO YA NJE YANAWEZA PATIKANA KUPITIA NJIA HIZI
1. kupitia maonyesho mbalimbali ya kibiashara yanayo fanyika katika nchi hizo- haya maonyesho mara nyingi yanakutanisha wauzaji na wanunuzi so ndo moja ya maeneo mwafaka ya kupata masoko,
2. Kupitia website za kibiashara za makampuni mbalimbali
3.Ziara binafisi ya wewe mwenyewe kwenda kutafuta masoko, kwani hata wao huwa wanakuja kutafuta masoko huku kwetu directilly