Je, ni biashara gani Mtanzania anaweza kuifanya nje ya nchi (export)?

Mkuu Chasha heshima yako kamanda.

Mimi kwa kuishi ughaibuni nimegundua baadhi ya bidhaa ambazo zikishughulikiwa kikamilifu kwenye branding na packaging zinaweka kumtoa mtu.

1. Tumbaku wazungu bado wanapiga sana sigara

2. Kahawa- kahawa bado inauzwa sana na maduka migahawa mikubwa kama starbucks, costa café na wengine.

3. Vinyago vya aina mbalimbali.

4. Bidhaa zingine kama vikapu ambavyo wazungu akina mama wanapenda kutumia kufanya shopping ila view vimeshonwa kwa ufundi wa maana.

Vingine ntaendelea.
 
Msaada kuhc soko la sembe(unga wa mahindi )kwa nchi kama Uganda...imekaaje hii wadau...???
 
Msaada kuhc soko la sembe(unga wa mahindi )kwa nchi kama Uganda...imekaaje hii wadau...???

Hiyo itakulipa sana kama una processing machines na pia unafanya packaging ya uzito mbalimbali mfano 5kg, 10kg , 20kg.
 
Cc Invisible hii thread muhimu sana katika kuwafumbua macho wabongo ili nao wafaidi masoko ya nje nimeona ni muhimu uka weka kama sticky thread.
Cha ajabu thread muhimu kama hii watu hawacomment..Wamejaa tu huko kwenye siasa kuanzisha thread za kuombea majanga yatokee TZ. Vitu kama hivi vya msingi ambavyo vinaweza kuwa na faida kwao binafsi na nchi yao hawana habari navyo
 
Bidhaa zingine ambazo mtu anaweza ku-export Ulaya:

1. Raw Skin na hii imegawanyika wanaweza kutaka tanned au iwe salted kulingana na aina za wanyama.

2. Ngozi yenye manyoya nazo zina grades

3. Mchele ambao unaweza kushindana na ule wa Mali Rice au Dragon Rice wa Thailand.

4. Korosho roasted au zilizokaushwa maana zingine zinatumiwa hadi kupikia vyakula kama pilau za aina mbalimbali, hizi zinaweza kuwa shelled au inshell.

5. Asali iwe nzito au laini.

Kuna nchi kama Uingereza unatakiwa uwe umejiandikisha kwenye mfumo wao wa uingizaji bidhaa unaitwa CHIEF System ambao bila huo hujaingiza kitu nchini humo.

Ni mfumo wa kudhibiti imports kutoka nje ya bara la Ulaya.
 
HAO JAMAA KUFANYA NAO KAZI NI NGUMU AISEE HASA VYAKULA.MI BINAFSI HUWA NAWAGWAYA,BORA NIPIGE BUSINESS NA WATU WA ASIA MAANA WANA AFADHALI KULIKO HAWA WEUPE.
 
good thread!!!
kuna haja ya kuunganisha nguvu kwa hili tuweze fika mbali kama jirani zetu. wanao export tunaweza kushirikiana sisi wengine ni wakulima
 
good thread!!!
kuna haja ya kuunganisha nguvu kwa hili tuweze fika mbali kama jirani zetu. wanao export tunaweza kushirikiana sisi wengine ni wakulima
Kabisa,wazo zuri
 
Jamaaa unajua matatizo yote ila hujui hata suluhisho moja
 
Umejitahidi kuchambua vizuri sana mkuu,na hapa ndipo tunapokuja kuona tunahitaji kuwa na raisi mwenye dira na sio mkurupukaji na mwenye mawazo ya visasi na kukomeshana.

Imagine ndege moja ingeweza kujenga maabara ngapi za kilimo?walau tu kukawa na hata kanda zisizopungua 5 ambapo wakulima wangeweza kulima mazao yanayoendana na ardhi walizonazo ktk maeneo yao,Au pia magonjwa mbalimbali yangekuwa na tiba sahihi baada ya kujulikana tofauti na sasa wakulima wanabahatishabahatisha tu kwa kujaribu jaribu madawa.

Tunazalisha bidhaa za kilimo kwa gharama kubwa ukianzia kwenye vitendea kazi(mashine) makodi kibao kuanzia shambani hadi sokoni hapo bado wataalamu wachache ambao nao wana utaalamu mdogo na wanafanyia kazi maofisini ukitaka umpwleke shamba mpaka umtafutie usafiri.

Dah kweli mambo ni mwngi na muda ni mchache.(By Juma Kapuya)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
natumaini serikali sikivu imelifanyia kazi wazo langu, katika kikao kilichopita cha ma ceo kule arusha, serikali imetamka ita support mashirika yatakayowekeza nje ya tanzania, na kwa sasa tayari crdb waneshafungua matawi congo na burundi na yanafanya vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…