Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Hata Minara wanakodi
Wafanyakazi wameoutsource kwa watu.
Wanafanya hivyo kuepuka mambo mengi.
Hawajengi sababu assets zao zaweza dakwa na serikali

I see

Kumbe ni uamuzi wakimkakati sio kwasababu ya uwezo
 
Hiyo nyumba itarejesha hela yake baada ya miaka 21
 
Mi naona kupanga saa zingine ni vizuri kuliko kwenda jenga mbali unatumia gharama kusafiri na muda unapoteza mwingi.
Mtu anaishi Bunju anafanya kazi Posta huyu alitakiwa apange kkoo ili apunguze muda unaopotea na fedha anazotumia kwenye usafiri

Hii ni point ya msingi ambayo watu wengi wanaisahau na inawaumiza sana
 
Kujenga nyumba 150M then kupangisha kodi ya 400k ni maamuzi mabaya ya kiuwekezaji hata kama unatarget mbali kwa strategy ya kukusanya pango bado hailipi.

Utamaduni wa ya afrika ni kukumbatia nyumba ila kwa hizo pesa, kma unataka kuzizalisha strategy nzuri ni kujenga na kuuza au kununua na kuuza nyumba. Ukizungusha ndani ya miaka 5 utakuwa umedouble hyo pesa au zaidi.

Ila sasa naona kma soko la nyumba na real estate kwa bongo limeshuka sana.
 

Mawazo mazuri sana hasa kwakua yameeleza pros and cons na kutoa maangalizo
 
Hujamuelewa labda usome kuanzia story za mwanzo hapo juuu, ukifanyia biashara 150.000.000 ndani ya miaka mitano utakuwa umeishapata zaid ya 600.000.000
Biashara nayo ni fani siyo kila mtu ana fani ya biashara. Ushauri niliotoa ni kuwa kama wewe una biashara yako ina thamani ya TShs 250,000,000 na wewe unahisi mtaji wa 100,000,000 unatosha kuendesha biashara yako; toa ile 150,000,000 ukawekeze kwenye nyumba.
 
Future ni unpredictable ndugu. Nani alijua kuwa fremu za biashara kariakoo zitakuwa obsolete miaka ya hv Karibuni? Watu walikwenda na upepo wa bandari mpya ya Bagamoyo wakanunua Maeneo huko Mlingotini na njia ya Msata kiko wapi?

Umetoa angalizo zuri sana mkuu

Business models are changing ni lazima na sisi tuchange
Nani alijua kwamba Taxi zitakuja kua obsolete sababu ya Uber
Mauzo ya magari yatapungua sababu ya uber
Maduka yatakuja kua obsolete kwakua watu wananunua online na kufanyiwa home delivery
Benki nazo zisipoangalia zitakuja kua obsolete now that mobile money is booming
Very soon western union na money gramm zitakua obsolete watu wanatumai wave
Michepuko yakudumu inakua obsolete kwasababu ya Escort services kama exotic

Nakadhalika
 

UShauri makini sana huu na angalizo zuri sana. Bravo
 
Kiwanja maeneo yaliyochangamka utanunua kwa pesa ngapi?unafahamu kwamba maeneo ya nje ya mji Kama Tegeta au Kimara maeneo karibu na barabarani hiyo pesa yote inaishia kwenye kiwanja?
 
Financial Literacy tuipate wapi? Au ile inayotolewa na Dr. Mauki (PhD)?
 
 
Kwanza. Mfanyabiashara au mfanya kazi, Ogopa sana kujenga nyumba kwa hela ya mkopo benki. itakutesa sana nyumba jengea hela ya faida au hela ya mshahara pasipo mkopo. Pili sio jambo baya kujenga nyumba ya kupanga unatakiwa utumie akili tuu nyumba pangisha laki 6 au kodi yoyote utakayo ona ipo relevant na nyumba yako, halafu hati ya nyumba kakopee benki upate hela za biashara utakua umewaza kama kocha. Risk ya hasara iliyopo kwenye nyumba ni ndogo sana compared to kwenye biashara, imagine umekopa benki milioni 100 umeingiza 70 kwenye biashara ya nguo ma agent wa bandarini wakakutapeli ukala hasara au hela ikapotea yote ukabaki na 30 unaona ujenge na 30 hiyo hunakiwanja, bado mafundi hawajakuibia endapo umeanza kujenga. so kila kitu kinafaida yake na hasara yake japokua hasara ya biashara ni kubwa kuliko ya nyumba( nyumba kama italipa taratibu lakini ni lazima utapata hela) biashara ina mwezi wa kismati. so akili kumkichwa amua unalo ona linakufaa
 
Portfolio. Usiweke mayai yako yote kwenye kapu moja.

Passive income: Nyumba ya kupangisha na investments nyingine kwa kiasi kikubwa ni passive (haihitaji uwepo wako ili kuleta income....hata ukiwa mahututi kitandani income yako ipo pale pale). Kwa hivyo unapolinganisha investment na business income ni vema kuzingatia hili pia.

Yote kwa yote, jaribu kuchanganya aina za vipato.....biashara (various) na investments (various). Usitegemee biashara pekee au biashara moja au invement pekee au investment moja. Kuwa na nyumba, FDR, shares, bonds za serikali etc. Lakini pia kuwa na biashara pia.....inasaidia kuzubgusha pesa kwa haraka.
 
Nashauri mkopo chukua ukiwa umeanzisha kitu na kimebaki asilimia chache kuwa kimekua au kimekamilika. Mfano nyumba jenga kwa pesa zako cash sio mkopo jenga mpaka ifike asilimia 80 kopa its okay. Kwa biashara, hakikisha imesha anza na imeshafahamika na wateja na ina mtaji wake, hapo kopa uiendeleze utaona faida. Siyo mtu unakopa hela za kujenga huna kiwanja huna boma la nyumba wala huna ramani ya nyumba. Unakopa huna hata kibanda cha biashara utaaibika mjini. Kopa hela fanyia finishing nyumba yako hela inabaki unafanyia biashara, kopa hela weka kwenye biashara inayo exist ili uiboost. siyo unakopa hela unanunua gari.
 
Mimi nimejifunza kucheza na FDR ambayo ukipata say 12% kwa 150m inalipa kuliko nyumba ya kupanga. Hivyo fedha yangu inagawanyika FDR na Fixed assets plus other sources of income. Hapo unaishi comfortable life tu. Kifupi nyumba ya kupangisha ya say 200m repayment yake kwa kodi ni miaka kadhaa but nikicheza na hiyo 200m kwa FDR nakuambia kuzalisha another 200mm ni muda mchache zaidi.
 
Wahindi wengi nchini hawamiliki nyumba ila wamefikia utajiri wa kutisha. Sisi wabantu tunakimbilia kujenga Mapinga, sijui Mkuranga watoto tunawapeleka st.kayumba bado utegemee maajabu maishani
Hao wahindi unaosema hawajengi bongo ni washenzi sana wao wanajenga Canada na Uingereza Tz kwao ni kama shambani tu utajenga shambani?
 
Points tupu. Mimi financial market ndiyo iliniinua kuliko hata hizo kodi za nyumba. Shares kuna maeneo niko vizuri ila mengine tunachechemea ila ndiyo kamari zenyewe. Nyumba kwa sasa na suffer kodi zimeshuka sana na wapangaji wanajijengea hivyo hii market kwa DSM inaanza kuyumba. Kifupi ni kutawanya mayai kwa kapu mbalimbali kama uwezo upo. Ila aisee ukiwa na mkwanza mzuri ukiuserka FDR say 1bn kwa 120m inalipa kwa sasa kuliko kodi za nyumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…