Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

FDR ndio fixed deposit ?
 
150m unajenga apartment 6 kila moja kodi 250000 kwa mwezi hapo ndipo utaona faida ya nyumba
 
Case ya Kariakoo ni very unique and rare. Wote hapa tunajua nan kavuruga uchumi wa nchi na kupelekea hali hiyo, sema tu tunaogopa kumtaja. Ndo hapo utajua biashara ni siasa. So kuwa na imani, hii hali itabadilika 2026.
Dah,amevuruga then yeye binafsi cant feelz, neibour situations / huku twafaa jamaa...The country is not bisiness friendly at all. Hata ueleze vipi haueleweki,tuvumilie tu hakuna jinsi tena.
 
Hivi kati ya nyumba na land kipi kina appreciate na kipi kina-depreciate with time ?
 

Ushauri makini sana kwa kizungu wanaita learned advice na wala sio layman
 

Sahihi kabisa

Mkuu uko makini na una uelewa mkubwa sana
 
MKUU WENGINE TULIKIMBIA HESABU, NA KODI IKITOLEWA MWISHO MTU ANAPATA FAIDA GANI KWA MWAKA MMOJA AKIWEKA 2M?
Mfano umeweka mil 2 na tukitumia interest ya 7.5% ambayo ni ya mwaka mzima then itakua

2miliΓ—1Γ—7.5%(1-0.1)=Tsh. 135,000

So utapata laki moja na thelathini na tano hapo na kodi imeshakatwa tayari mkuu.
 
Tuseme baada ya miaka kumi umepata kiasi cha million 72. Je ukiamua kuiuza hiyo nyumba utapata kiasi gani? Million 200 au hata 300. Jumlisha na ile 72?
Thamani ya nyumba/ardhi huongezeka
Naomba kukurekebisha. Thamani ya Ardhi huongezeka kadri muda unavyosonga, bali thamani ya nyumba hupungua kadri muda unavyozidi kusonga. Jaribu kufikiria leo hii unajenga nyumba yako kwa sh 100M, je ukitaka kuiuza baada ya miaka 15 unadhani utauza utaiuza kwa zaidi ya 110 ?
 
... kwa mtaji huo jenga g/house/lodge unapata 30k daily per room; ukiwa na vyumba 20 unapiga 600k daily kwa mwezi almost 18m/- kabla ya kutoa gharama za uendeshaji (mishahara, utilities, etc.). Lakini it is far better.
Lakini kumbuka kupata wateja sio instantly lazima miaka hata miwili ndio utaona mzunguko mkuu.
 
Not in absolute terms. Most likely itaongezeka kutegemea iko wapi.
 
Mkuu nimeisoma vizuri hakuna tatizo kuwekeza kwenye nyumba kwa mkopo ilimradi uwe umepata eneo ambalo kuna wateja wa kutosha na isiwe nyumba ya kukaa mtu mmoja iwe ni appartments ili mzunguko wa fedha uwe unakwenda vizuri na uwe umeweka bei nzuri na huduma muhimu ziwepo
[/QUOTE]
 
Not in absolute terms. Most likely itaongezeka kutegemea iko wapi.
Leo hii nikijenga nyumba yangu kwa Mil 50. Mpaka inafika miaka 10 au 15 mambo mengi sana yatakuwa yamebadilika; Nitatakiwa kufanya marekebisho pale itakapohitajika, teknolojia kwenye suala zima la ujenzi zitakuwa zimebadilika kitu kitachofanya materials nyingi nilizotumia katika ujenzi wangu kuonekana sio za kisasa tena( mfano nyumba yangu niliezeka bati za Champion leo hii katika ulimwengu wa mabati ya Rangi kama rangi kama Romantile, Versatile, Tekdek lazima nyumba yako ionekane ina bati la enzi za ukoloni pengine ukute bei ya bati kwa wakati huo inaendana kabisa na hii ya sasa kwa kiwango cha Rangi),design ya nyumba yako nayo pia inaweza ikawa ishapitwa na wakati kitu kitachofanya nyumba yako ionekana sio ya thamani hiyo ambayo unataka kuiuza.

Hivyo basi, ili nyumba yako iwe na ubora wa kuuzika kwa wakati huo lazima uipandishe hadhi kitu ambacho kitakulazimu uingie gharama nyingine.
 
naamini kuwa watu wengi hukimbilia kujenga sababu aidha ya uoga ama kutokuwa na elimu ya biashara hivyo ujenzi wa nyumba ya kupngisha haihitaji ujuzi tele kuweza isimamia..

ila nyumba ni uwekezaji poa sana ukiufanya kwa umakini.
usiitegemee pekee kiwe chanzo cha kipato chako kwani kwa hasa sisi wa kipato cha chini matunda yake utaanza yaona huko mbeleni..
hiyo 150m ukiiwekeza kwenye FDR,Bonds & Units naamni italeta return kubwa zaidi..ila ujenzi pia ni muhimu sana sana!

yote ya yote USIWE NA CHANZO KIMOJA CHA MAPATO!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…