Je, ni dhambi au si dhambi,kujipamba miili kwa wanawake wa Kikristo?

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
611
Reaction score
993
JE!? ni dhambi au si dhambi kwa kujipamba miili kwa wanawake wa Kikristo.
yaani kusuka nywele za mkono au mawigi
kuvaa mapambo kutoboa sehemu za miili yao na kuvaa hereni na vikukuu
kuvaa mavazi ya kiume au yanayoacha wazi sehemu za miili yao,nguo zinazowabana na kuchora maumbile yao au nguo zinazoangaza kuonyesha michoro ya nguo za ndani,
kuvaa kupaka make ups,wanja,kujichubua rangi ya ngozi,kuvaa vitu bandia kama kucha,kope,rangi ya midomo,kufanya upasuaji wa kurekebisha kuongeza au kupunguza muonekano maumbile ,n.k

View: https://youtu.be/pEARlkOVkaA?si=zq6nU5DPjxPJx7KM

Ngoja tuwasubiri wakolosai wa Samvula Chole waje
 
Siku zote nia ya kutenda kitu au jambo fulani ndiyo linalokuhukumu. Waisraeli walichukua mapambo ya dhahabu ya wake zao na kumpa Haruni akatengeneza ndama waliyemuabudu. Kosa siyo yale mapambo, ila matumizi ya yale mapambo. Hali kadhalika Mfalme Suleiman alijenga Nyumba ya Mungu (Hekalu) kwa kutumia miti, fedha, dhahabu, n.k. yakiwemo mapamba ya wanawake Waisraeli. Suala ni unakusudia nini kufanya kutokana na mapambo hayo!
 
JE!? ni dhambi au si dhambi kwa kujipamba miili kwa wanawake wa Kikristo.
yaani kusuka nywele za mkono au mawigi
kuvaa mapambo kutoboa sehemu za miili yao na kuvaa hereni na vikukuu
kuvaa mavazi ya kiume au yanayoacha wazi sehemu za miili yao,nguo zinazowabana na kuchora maumbile yao au nguo zinazoangaza kuonyesha michoro ya nguo za ndani,
kuvaa kupaka make ups,wanja,kujichubua rangi ya ngozi,kuvaa vitu bandia kama kucha,kope,rangi ya midomo,kufanya upasuaji wa kurekebisha kuongeza au kupunguza muonekano maumbile ,n.k

View: https://youtu.be/pEARlkOVkaA?si=zq6nU5DPjxPJx7KM

View: https://youtu.be/pEARlkOVkaA?si=zq6nU5DPjxPJx7KM

Kama ulikuwa na mkataba au uliingia mkataba bila kujua au kwa ulaghai basi ujue utalipa tu! Mapambo ni vitu vya thamani ukiwa na tamaa ya kupata vitu vya thamani, mali, fedha, n.k. kwa njia rahisi rahisi, za mkato bila kujali uhalali wa upatikanaji ujue kuna viumbe wenye kutoa hayo yote. Mungu alimruhusu Ibilisi kuwajaribu wanadamu na wale anaowapata huwa ni mali yake ili aingie nao kwenye moto wa milele. Ukitumia njia halali Ibilisi hakugusi na ukimuomba Mungu bila kuchoka utafanikiwa kwa kadiri Mungu atakavyoona kiwango gani cha kukupa kitakachokufaa na muda gani wa kukupa. Wakati mwingine Mungu huwanyima watu au huwapa kwa kiasi kwa sababu anajua unaweza ukatumia kinyume na mapenzi yake. Ridhika na ulichonacho au unachopata, tamaa mbaya inamkaribisha Ibilisi.
 
Unahangaika na mijadala ya mapambo wakati mnaendelea kupigwa na manabii. Discuss more important issues
 
Kwa mujibu wa biblia mapambo ni dhambi.Wanaojipamba wanafanya hivyo kwa akili zao busara zao ila sinkwa msingi wa neno la biblia.(IPO NJIA IONEKANAYO KUWA NI NJEMA MACHONI PA MWANADAMU ILA MWISHO WAKE NI MAUTI).Hivi hata kwa akili ya kawaida tu MUNGU amekuumba ukiwa NATURALLY BEAUTIFUL) Mungu alipendezwa wewe uwe NATURAL hivyo ulivyo.wewe unaongeza mapambo ya bandia ARTIFICIAL lengo ili upendeze uongeze uzuri muonekano mzuri tofauti na ule wa asili Kwa maneno mengine unamsahihisha unamkosoa Mungu alivyokuumba(tatizo la afya ya akili ugonjwa wa akili huu) na kukosa kujiamini,mana unaamini vile ulivyo wewe hujakamilika.

Wanawake wanaovaa mavazi ya kiume kama suruali wanafanya hivyo kwa utashi wao sio kwa kufuata maandiko ya biblia.

HATA wachungaji wa kike na mama na watumishi wa Mungu,wanakwaya ,wazee wa kanisa,n.k nao wanapingana na biblia wanatafuta mistari ya kuunga unga kwwnye biblia kutetea kuwa eti MWANAMKE NINPAMBO,MARA NI UA,mara MUNGU haangalii nje ana angalia ndani roho ya mtu.MUNGU ANA ANGALIA NDANI NA NJE .Tena kama kwa nje tu unajipamba makucha bandia mawigi bandia n.k hata huko ndani unakojisifu rohoni unapotaka Mungu apaangalie ni most likely uwezekano pakawa bado ,maana ya ndani ROHONI ndio yanaonekana nje katika matendo./mwilini.
 
HILI LA MAPAMBO NDIO JANGA KUBWA LIMEKAMATA WENGI MPAKA NDANI YA KANISANI SHETANI ANAZIDI KUBUNI MAPAMBO MENGI KUTOKA KUZIMU NA KUYALETA KWA WATOTO WA MUNGU KAMA UREMBO/MAPAMBO ILI KUWAPELEKA WENGI MOTONI.
 
injili ya kweli isemwe ili watu wachague kuchukia dhambi zenyewe au wamchukie yule anayewaambia waache dhambi.
 
Attachments

  • images - 2024-12-27T230128.929.jpeg
    images - 2024-12-27T230128.929.jpeg
    21.7 KB · Views: 8
HILI LA MAPAMBO NDIO JANGA KUBWA LIMEKAMATA WENGI MPAKA NDANI YA KANISANI SHETANI ANAZIDI KUBUNI MAPAMBO MENGI KUTOKA KUZIMU NA KUYALETA KWA WATOTO WA MUNGU KAMA UREMBO/MAPAMBO ILI KUWAPELEKA WENGI MOTONI.
Ah wapi, mambo mengine mpunguzieni shetani. Wakristo wanajijaza ujinga kila siku utasema magari ya taka taka and then you come here raising light topics za mapambo? Eti mapambo kutoka kuzimu. Ipi hiyo? Mie nipake rangi niende motoni wewe uwapige watu 3 million kukuona afu uende peponi.😂
 
Kwa mujibu wa biblia mapambo ni dhambi.Wanaojipamba wanafanya hivyo kwa akili zao busara zao ila sinkwa msingi wa neno la biblia.(IPO NJIA IONEKANAYO KUWA NI NJEMA MACHONI PA MWANADAMU ILA MWISHO WAKE NI MAUTI).Hivi hata kwa akili ya kawaida tu MUNGU amekuumba ukiwa NATURALLY BEAUTIFUL) Mungu alipendezwa wewe uwe NATURAL hivyo ulivyo.wewe unaongeza mapambo ya bandia ARTIFICIAL lengo ili upendeze uongeze uzuri muonekano mzuri tofauti na ule wa asili Kwa maneno mengine unamsahihisha unamkosoa Mungu alivyokuumba(tatizo la afya ya akili ugonjwa wa akili huu) na kukosa kujiamini,mana unaamini vile ulivyo wewe hujakamilika.

Wanawake wanaovaa mavazi ya kiume kama suruali wanafanya hivyo kwa utashi wao sio kwa kufuata maandiko ya biblia.

HATA wachungaji wa kike na mama na watumishi wa Mungu,wanakwaya ,wazee wa kanisa,n.k nao wanapingana na biblia wanatafuta mistari ya kuunga unga kwwnye biblia kutetea kuwa eti MWANAMKE NINPAMBO,MARA NI UA,mara MUNGU haangalii nje ana angalia ndani roho ya mtu.MUNGU ANA ANGALIA NDANI NA NJE .Tena kama kwa nje tu unajipamba makucha bandia mawigi bandia n.k hata huko ndani unakojisifu rohoni unapotaka Mungu apaangalie ni most likely uwezekano pakawa bado ,maana ya ndani ROHONI ndio yanaonekana nje katika matendo./mwilini.
Manukato pia ni mapambo, mwanamke alimpaka Yesu manukato/mafuta ya kunukia, lakini pia hata Yesu alipozikwa wanawake walienda kaburini asubuhi na mapema ili kupaka mafuta mwili wa Yesu ndipo walipokuta kaburi li wazi!
Unasemaje?
 
Manukato pia ni mapambo, mwanamke alimpaka Yesu manukato/mafuta ya kunukia, lakini pia hata Yesu alipozikwa wanawake walienda kaburini asubuhi na mapema ili kupaka mafuta mwili wa Yesu ndipo walipokuta kaburi li wazi!
Unasemaje?
 
Attachments

Unahangaika na mijadala ya mapambo wakati mnaendelea kupigwa na manabii. Discuss more important issues
No,swala la mapambo ni la maana kulijadili.
Pope Francis alifanya mkutano mkubwa na wauza vipodozi, presumably kuwaambia,"Keep it up. You are doing a good job "
Katika Buddhism wanawake walei( na wanaume walei) wanaruhusiwa kujipamba lakini monks and nuns are forbidden.
 
Ila sio kipaumbele. Narudia kusema kuwa Ukristo sasa hivi umeelemewa na maovu mengi kupitiliza. Hayo yangeangaziwa. Sishadadii mwanamke kutokuwa na stara ila Trust me, Mungu hasumbuliwi na hayo (kama anasumbuliwa)
 
Wanajipamba kwa ajili ya nani?

Wanajipamba kwa vigezo vya nani, nani anaoenda mapambo hayo, je huyo wanaye m-target anajua wanafanya hayo kumfurahisha yeye?

Je, wamewahi kumuuliza huyo wanayetaka kumfurahisha anapenda nini?

Wengi watasema wanajipamba kwa ajili yao, ni UONGO HIYO.
 
Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; [1 Timotheo 2:9]

Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; [1 Petro 3:3]
 
Back
Top Bottom