Wakuu habari ya uzima wenu,,,, namshukuru MUNGU kwa uhai na neema ya upendeleo kwetu,,atukuzwe MUNGU.
Basi bila kuchelewa Moja kwa moja kwa mada ,,,, tumekuwa na ubishi takiribani inakaribia miezi 6 jambo hili halijapata suruhu kati yangu na yule tuliyekuwa tumeanzisha mada hii, tumekuwa tukishirikisha watu mbalimbali ili kipata mawazo yao lakini kila mtu amekuwa na mtazamo wake kwa swala hili..
MADA:
Mfano; Mimi natoka eneo A kwenda eneo B na nauli yake kwa HAICE ni shilingi 700/= bei elekezi,,lakini mimi nikaomba kwa Kondakita kuwa nisaidie nina Tsh 500/= akaruhusu nipande baada ya mwisho wa safari natoa Tsh 1000 ama 2000,, Kondakita anakata 700 badala ya 500 niliyoomba ,,,
Je,Kondakita yupo halali kukata hiyo 700?!
Ama alipaswa akate 500 niliyoomba?!
UTATA:
Kwa upande wangu nilimtetea Kondakita kuwa yupo halali kukata 700,,,kwa maana me nimeomba anisaidie nina 500 ambayo siyo bei elekezi na sijampa maelezo yoyote kuhusina na hela niliyo nayo. Kwa maoni yangu ilipaswa niwe 500 iliyo jitegemea.
JAMAA YANGU:
Yeye anasema Kondakita anamakosa kukukata hiyo 700,,,ilitakiwa achukue 500 yake tu zingine arudishee,,,kwa maana yamkini kuna kitu ambacho anaenda kutumia kwa pesa inayo baki.
MADA HII IMEKUWA GUMZO
Kwenu wadau kwa maoni mbalimbali ili maada hii ipate suruhisho,,,niwatakie majukumu memaa!
πππ