Je, ni idadi gani ya watu waliowezesha mapato ya shilingi trillioni 3.1 kwa mwezi Septemba?

Je, ni idadi gani ya watu waliowezesha mapato ya shilingi trillioni 3.1 kwa mwezi Septemba?

KACK

Senior Member
Joined
Mar 28, 2015
Posts
129
Reaction score
107
Nawasalimu wote kwa jina la jamhuri ya Tanganyika.

Awali ya yote naipongeza TRA kwa kuvunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato kwa mwezi Septemba hadi kufikia Trillioni 3.1.

Pia nilishtushwa na taarifa za idadi ya watanzania wanaolipa kodi kwamba ni milioni mbili tu.

Hata hivyo ni jambo jema kwa upande mwingine, kwa sababu linatufungua macho na kupata mawazo zaidi ya kutafuta suluhu ya kitendawili hicho.

Binafsi nashauri kwamba; TRA kwa kuwa mnapata taarifa kama hizo za idadi ya walipa kodi nchini ni muhimu pia mnapotoa ripoti za makusanyo ya mwezi mfafanue yafuatayo:

1. Idadi ya watu wote waliochangia mapato hayo (Watanzania na wasio Watanzania)

2. Idadi ya waajiriwa waliolipa kupitia PAYE, taarifa idadavue waliopo katika sekta ya umma na sekta binafsi.

3. Tujue idadi ya waliolipa kutoka miongoni mwa ajira binafsi (Wafanyabiashara n.k)

4. Tujue sekta zilizochangia zaidi pato la taifa na zilizoburuza mkia.

5. Unaweza ongezea mambo mengine.

Kwa kila kundi tuambiwe wamechangia kiasi gani na tujue wastani wa makusanyo kwa kila kichwa kwenye kundi husika. Mfano tujue kati ya Trillion 3 zilizokusanywa, Watumishi wa umma walichangia biloni 900 ambayo ni sawa na wastani wa shilingi 180,000 kwa kila mfanyakazi.

Lengo la kufanya hivi ni kusaidia kuyafahamu maeneo muhimu yenye tija na yanayosuasua ili jitihada stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wakati.
 
Wanywa bia wako million 2 na ndiyo wachangiaji nambari wani.
 
Back
Top Bottom