Lukansola
JF-Expert Member
- Sep 5, 2010
- 5,435
- 1,604
haya waliotendwa tupene stori zenu.....
Haya ya kwangu hii hapa:
Nilikuwaga na my wife wangu, basi taratibu tabia yake ikaanza kubadilika, akawa anarudi hata saa nane usiku akiwa amelewa, hata siku yuko off anashinda bar tena ya jirani na home, analewa tu. Nilivumilia mpaka kiwango changu kilipofika mwisho. Wakati fulani mama yangu akaja kutusalimia kutoka mkoa. Demu hakubadilika, basi siku hiyo akaja amelewa kama kawaida lakini mapema kidogo saa tatu usiku, nilipomuuliza akawa mbogo, nikajikuta nimesha mtwanga kofi lililompeleka mpaka chini, aliponyenyuka hapo akaingia chumbani akachukua cheti chetu cha ndoa akakichana mbele ya mama yangu mzazi halafu vipande akamtumpia hapo chini akaondoka kwenda kuendeleza gambe. Kitendo hicho sijakisahau, ingawa hakiniumizi tena.