k2206
JF-Expert Member
- Apr 22, 2018
- 702
- 705
WAKUU ,natumuani mu wazima wa Afya. Karibuni mtoe mchango wenu kwa kina kuhusu hizi forwarding companies za vifurushi kutoka mataifa mbalimbali kama vile USA,UK,n.k.
Mimi nimekuwa nikifuatilia baadhi ya makampuni Kama vile,MYUS,STACKRY,SHIPITO,COMGATEWAY na,VYKINGSHIP kuhusu aina za bidhaa wanazosafirisha.
Kitu ambacho nashindwa kuelewa moja kwa moja ni kuhusu Kama wanasafirisha bidhaa zenye betri hasa za aina ya Lithium ion Kama simu,laptops,tablets,digital camera,saa n.k.au la.
Japo Kuna bidhaa nyingi ambazo zinajulikana Kama Ni hatari na haziruhusiwi kusafirishwa kimataifa kulingana na Sheria za nchi mbalimbali zinapotoka,au zinapokwenda,au kulingana na sheria za kampuni husika,bado Kuna kigugumizi kuhususiana na hizi bidhaa zenye betri.
Ninaomba yeyote humu ndani anayejua kampuni inayosafirisha hivi vifaa vyenye betri atueleze. Pia atufafanulie kuhusu gharama za hiyo kampuni Kama zipo juu au la ukilinganisha na makampuni mengine ambayo ameshawahi kuyatumia.
Ahsanteni na karibuni kwa michango yenu ya MAWAZO.