Je, ni kampuni gani ya kusafirisha vifurushi ambayo inakubali kusafirisha bidhaa zenye betri kama vile simu na computer?

Je, ni kampuni gani ya kusafirisha vifurushi ambayo inakubali kusafirisha bidhaa zenye betri kama vile simu na computer?

k2206

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2018
Posts
702
Reaction score
705
WAKUU ,natumuani mu wazima wa Afya. Karibuni mtoe mchango wenu kwa kina kuhusu hizi forwarding companies za vifurushi kutoka mataifa mbalimbali kama vile USA,UK,n.k.

Mimi nimekuwa nikifuatilia baadhi ya makampuni Kama vile,MYUS,STACKRY,SHIPITO,COMGATEWAY na,VYKINGSHIP kuhusu aina za bidhaa wanazosafirisha.
Kitu ambacho nashindwa kuelewa moja kwa moja ni kuhusu Kama wanasafirisha bidhaa zenye betri hasa za aina ya Lithium ion Kama simu,laptops,tablets,digital camera,saa n.k.au la.

Japo Kuna bidhaa nyingi ambazo zinajulikana Kama Ni hatari na haziruhusiwi kusafirishwa kimataifa kulingana na Sheria za nchi mbalimbali zinapotoka,au zinapokwenda,au kulingana na sheria za kampuni husika,bado Kuna kigugumizi kuhususiana na hizi bidhaa zenye betri.

Ninaomba yeyote humu ndani anayejua kampuni inayosafirisha hivi vifaa vyenye betri atueleze. Pia atufafanulie kuhusu gharama za hiyo kampuni Kama zipo juu au la ukilinganisha na makampuni mengine ambayo ameshawahi kuyatumia.

Ahsanteni na karibuni kwa michango yenu ya MAWAZO.
 
HIZI NI BAADHI YA BIDHAA AMBAZO HAZIRUHUSIWI KUSAFIRISHWA KUTOKA KWA KAMPUNI YA STACKRY.
Asbestos

Wastes as defined in the IATA regulation

Garbage

Disinterred human remains

Corrosives

Combustible material

Lithium Batteries*

Human remains, including ashes

Embryos

Learn more about hazmat here!

HAPO KWENYE LITHIUM BATTERY KUNA NYOTA. SIJUI INAMAANISHA NINI.

Lakini pia Kuna ishu ya hazmat{hazard materials} ambayo Ni material ambayo hutakiwa kusafirishwa kwa uangalizi mkubwa maana huweza kuhatarisha maisha ya wahudumu,au vyombo vya usafirishaji. Kwa hiyo inatakiwa kumpa taarifa carrier kuhusu hiyo bidhaa Kama Ni hazmat ili aweze kuihandle na kuipack kwa ungalifu mkubwa.

Baadhi ya hizo hazmat Ni;
_lithium batteries,
_electronic equipment zenye lithium batteries Kama simu,tablets,laptops,smartwaches,etc.

_car batteries,
-carbondioxide containers and cylinders,
_flammable chemicals etc. Ingia STACKRY kwa maelezo zaidi.

Swali Ni kwamba wanasafirisha hizo bidhaa au hawasafirishi?
Kwa wanaoelewa haya Mambo watuelekeze ili tuweze kujua Ni makampuni yapi yanaruhusu maana wengi wetu tunapenda sana hizi electronics zenye lithium battery kuzitumia na kuziagiza.
NB;

Haya maaelezo nimeyatoa kwenye kampuni ya STACKRY.
KARIBUNI SANA.
 
Back
Top Bottom