SoC04 Je, ni kipi kianze uhuru wa kiuchumi au uhuru wa kujieleza? Timu ya Usimamizi wa Uchumi

SoC04 Je, ni kipi kianze uhuru wa kiuchumi au uhuru wa kujieleza? Timu ya Usimamizi wa Uchumi

Tanzania Tuitakayo competition threads

ANQAA

New Member
Joined
Apr 21, 2020
Posts
4
Reaction score
2
Munakasha wa kipi kianze kati ya vitu hivyo viwili umekua ni endelevu na wa muda mrefu na mgumu. Aina zote mbili za uhuru ni misingi ya jamii za kidemokrasia na maendeleo binafsi na taifa kwa pamoja. Ila linapokuja swali la uhuru upi upewe kipaumbele, jibu linakua gumu na si la moja kwa moja.

Tanzania kama mojawapo ya Nchi zinaoendelea imejikuta ikiwa katika mtanziko kama huu. Kila Raisi anapoingia hujikuta ima anakitanguliza kimojawapo au anakibananga kimojawapo. Si lengo langu kuchambua itikadi tofauti tofauti za kiuongozi katika awamu mbalimbali Ila nitakua ninadonoadonoa mifano kutoka katika awamu mbalimbali ili kuweza kujenga ni nini nakitaka mbele.

Uhuru wa kiuchumi huusisha haki ya msingi ya umiliki wa mali, uendeshaji biashara kwa uhuru na uwezo wa kutumia rasilimali mbalimbali pasina vizuizi. Uhuru wa kujieleza humaanisha uwezo wa watu kutoa maoni binafsi pasina hofu ya kukamatwa na serikali au kukagiliwa.

Japokua dhana hizi mbili zinatofautiana Ila zinaendana sana. Tanzania imewahi kufanya majaribio ya kujenga uchumi katika misingi uhuru mdogo wa kujieleza huko wakati wa azimio la Arusha, majaribio ambayo yalifeli vibaya sana na kupelekea kuingizwa kwa azimio la haki za binadamu katika katiba.

images (6).jpeg

Kwa hisani ya maktaba.org​

Hii inamaanisha kua Ili kupata uhuru wa kiuchumi uhuru wa kujieleza ni muhimu. Na mifano ni mingi sana katika hili hata nje ya Tanzania. Hebu tujiulize kuanguka kwa Dola ya usovieti na mataifa ya Ulaya mashariki. Mtu anaweza kutoa hoja "mbona China haina uhuru wa kujieleza na imepiga hatua kubwa sana"?

Jibu ni moja, kua modeli hiyo ya kiuchumi na kimaendelo ni yenye kuacha maswali mengi kuliko majibu. Na inaweza kua si endelevu na hivyo si nzuri kuigwa na Nchi kama Tanzania. Awamu ya Tano ilijaribu kutumia sehemu ya modeli hiyo katika kuyafikia maendeleo Ila nayo ilifeli maana si modeli endelevu.

Awamu hii imejaribu kufanya maboresho kuongeza kidogo sana wigo wa uhuru wa kujieleza, Ila bado haujafikia kiwango kinachohitajika kuweza kupata matokeo ya uhuru wa kujieleza.

images (5).jpeg

Kwa hisani ya Jamiiforums.com​

Je Tanzania niitakayo ni hii? Ambayo kiongozi akihoji jambo la kiuchumi anaishia kujiuzulu pasina kutoa sababu madhubuti kwa waliomchagua? Au raia wa kawaida anawekwa mahabusu? Bila shaka sio hii.
Tanzania niitakayo ni Ile ambayo Ina uhuru wa kujieleza na kutoa maoni kuufukia uhuru wa kiuchumi. Katika mrengo huo huo utoaji wa maoni ya kuujenga uchumi yanatakiwa kua jumuishi, hivyo ningeenda kuiangazia Tume ya mipango chini ya Ofisi ya Raisi.

Ili kuhakikisha Hilo kuundwe Timu ya usimamizi wa uchumi'Economic Management Team". Hii Timu inatakiwa ijumuishe watu wenye uzoefu mkubwa kutoka serikalini na sekta binafsi. Ujumuishaji wa watu kutoka sekta binafsi unaweza kuonekana kama unaweza kuzaa mgogoro wa kimaslahi. Ujumuishaji huu wa sekta binafsi utasaidia kuleta uzoefu kutoka sekta binafsi na sekta binafsi zitaweza kufahamu kwa haraka madhumuni ya serikali kufanya mabadiliko mbalimbali na hivyo kuongeza kukubalika kwa wepesi sera mpya kwa wepesi.

Timu hii iundwe na Raisi Kama mwenyekiti wake, mawaziri kutoka sekta muhimu zote za kiuchumi, mshauri wa raisi (Uchumi), mshauri wa raisi (Tathimini na Ufuatuliaji),viongozi wa taasisi za kifedha za umma kama gavana wa benki kuu, Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato, Msajili wa hazina, spika, viongozi kadhaa wa sekta binafsi na wengine ambao wataonekana wanafaa. Kwa kua Timu hii itakua kubwa sana, basi kunaweza kuundwa Timu mdogo kwa ajili ya utendaji wa kila siku. Kwa hiyo tume ya mipango ya sasa inaweza kutumika kuunda tume ndogo.

Hii itatoa wigo mpana wa watu kuhusika na kuujenga uchumi badala ya kutegemea watu wachache sana waliohodhi Mamlaka ya kuendesha na kushauri masuala ya kiuchumi.

Itaongeza wigo wa wananchi kujihisi wapo kwenye uelekeo sahihi. Na hii itaepusha kusigana kati ya Ile mihimili miwili juu ya ongezeko la deni la taifa.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom