Je, ni kwanini leo mabenki yote ya biashara Tanzania hayataki kuikopesha Serikali kama ilivyokuwa wakati Hayati Rais Magufuli?

Mwanahabari wa Taifa

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2020
Posts
1,588
Reaction score
956
Your browser is not able to display this video.

Sikiliza hii kwa makini mpaka mwisho

Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali kwake wanyonge imeendelea na jitihada zake za kuwapunguzia riba wakopaji wadogo wakati na wakubwa (MSEs, SMEs & Cooperate)

Akihojiwa na kituo cha Utangazaji cha E-FM redio, Mkuu wa Mkoa Simiyu Mhe David Kafulila amefafanua kwanini mabenki yameikimbia serikali kwenye mikopo na badala yake yameelekeza nguvu kwa Watanzania wanyonge, Kafulila anasema,

" Hoja ya kukopa sana ndani kiasi cha kushindana na sekta binafsi ni dhaifu sana kwenye mazingira ya awamu ya sita kwasababu serikali inakopa kwa riba ndogo kiasi cha asilimia 4-5% kwa hatifungani za mwaka mmoja,

Kuna miaka huko nyuma tulipata kukopa soko la ndani kwa hatifungani za mwaka1 kwa riba ya asilimia 17,

Hapo hoja ya kukopa ndani kiasi cha kufanya bank zitamani kufanya biashara na serikali tu ilikuwa na uzito.

Kwani kama serikali inakopa ndani kwa riba 17% kwa hatifungani za mwaka1, niwazi bank zitapandisha zaidi riba kwa sekta binafsi kwa kati ya asilimia 22% mpaka 23%.

Hii sio Serikali 'desperate' hata ishindane na sekta binafsi kukopa ndani. Hata hali ya deni inaonesha hivyo kwamba deni la ndani ni kama asilimia 30% ya deni lote.

Ndio maana ni Rais SSH alielekeza Bank kuu( BoT) kutenga trilioni1 kukopesha bank za biashara kwa riba ya chini kimkakati ili bank hizo zikopeshe sekta ya kilimo kwa riba isiozidi 10%.

Hii ni 'stimulus package' kabisa kwenye kuinua sekta ya kilimo. "- David Kafulila
 
mambo ya mumeo yanatoka wapi tena?
 
Huyu mtu ni kichwa sna
 
Uchambuzi huu ni wa kitaalamu Sana
 
Wakati wa Magufuli Mabenki yaliuza nyumba za watu balaa,
Mikopo ilikuwa hailipiki,
Leo chini ya Mama Samia kila kitu "good "
Wewe nae huishia kukurupuka. Aishi.

Magufuli alishusha sana riba. Kasome Tena ili kichwa kichangamke maana unatia aibu.

Hapo Kafulila kaingelea kipindi akiwa bungeni. Yaani kabla ya 2015.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…