Je, ni kwanini Millard Ayo na Mkurugenzi wa TANAPA wasishtakiwe kwa uhujumu uchumi?

Je, ni kwanini Millard Ayo na Mkurugenzi wa TANAPA wasishtakiwe kwa uhujumu uchumi?

Tanapa waliwe kichwa kwanza kwa hilo, lakini si kila taarifa ni ya kupost. Hivi mtu mwenye followers milioni 14+ unashindwa kutumia busara kujua kwamba hiki sio cha kusambaza kwa maslahi mapana ya nchi? Hao watalii wakishajuwa mbuga flani kafa mtalii, mentality yao itabadilika, na watapungua..
Huna hoja kaka, wasinge post wao wangepost wageni, au familia ya mfiwa. Na hii si mara ya kwanza ajali kutokea.
Mamlaka imefanya sawa kabisa, punguza ushamba na mihemko
 
Lakini wasingejua kwa wingi wa kiasi hiki, kuna vitu vingi vyenye negative impact kwenye utalii ambapo huko kwa wenzetu huwa vinabaki minong’ono tu, lakini hawatangazi wala kudhibitisha…
Kwa wenzenu wapi wasitangaze umeenda Nchi gani ajali itokee wakae kimya wewe kila kukicha ni huyu akamatwe huyu ashtakiwe mnawaacha Majambazi wakubwa wakitafuna fedha za Serikali hivi kweli unafikiri kabisaa kwamba wazungu wasijue wewe msaga nyoka ujue?
Ajali ya Mv Bukoba tulikua tunadanganyana kuwa sijui meli ilijaza mzigo mkubwa wakaja USA wakasema Meli hii hapa imegonga mwamba ndio chanzo cha ajali..
Watengeneze hizo bara bara ndio chanzo kikubwa cha ajali huko na zinatokea mara kwa mara wasifikiri kukusanya dollar tu..
 
Hiyo habari ni kweli au siyo kweli? Kila siku tunasikia habari za ajali za ndege za Boeing na bado zinafanya kazi kama kawaida japokuwa wana historia mbaya katika safari zao.

Hii nchi ina watu wajinga-wajinga sana, kila kitu mnataka kuweka siasa.
Tena hayo mandege yalishafanyiwa na uchunguzi na kuna baadhi ya nchi yamepigwa marufuku. Mengine kurudishwa kiwandani.

Siasa kwenye kila kitu haifai. Na ajarizinatokea kila sehemu muhimu kufanya uchunguzi kama kuna uzembe alio husika achukuliwe hatua
 
Avatar yako inasema mengi kuhus ww, endelea kuamini katika kuficha taarifa
 
Sote tunafahamu umuhimu wa utalii kwenye kuchangia pato katika uchumi wa nchi yetu. Hivyo basi, panapotokea taharuki inayoweza kusababisha kupungua kwa idadi ya watalii, anayesambaza hiyo taharuki ni sawa na mhujumu uchumi tu.

Sasa kulikuwa na haja gani kwa hawa watu wawili kupiga makelele na kuitangazia dunia nzima kwamba kuna mtalii amekufa kwa ajali ya gari huko mbugani, lengo ni nini hasa?


View: https://www.instagram.com/p/C9-6AXZiYk1/?igsh=YW5teWp0aG54aWpm

Kwamba Miladi ashitake kosa gani?
 
Kila mtu anaangalia maslahi yake, Millard kuitoa hiyo taarifa inazidi kumweka vizuri na anavuna mashabiki nje na ndani ya nchi.

Suala la kusema maslahi mapana ya nchi walitakiwa waanze wenyewe viongozi wa nchi na wakusanyaji kodi.
Kila mtu angekuwa anaangalia maslahi yake binafsi bila kujali madhara makubwa yanayoweza kutokea at large sidhani kama kuna nchi ingepiga hatua hapa duniani, lazima pawe na hisia za uchoyo wa maendeleo, kama ilivyo Kenya. Kama serikali imekosea sio lazima na wewe umalizie kabisa kuharibu.., ni akili ndogo tu ilihitajika..
 
Back
Top Bottom