Je, ni kwanini TRA isibinafsishwe ili kuongeza tija na ufanisi katika ukusanyaji mapato?

Je, ni kwanini TRA isibinafsishwe ili kuongeza tija na ufanisi katika ukusanyaji mapato?

Tra wapewe waarabu sisi imetushinda kwa kweli mzigo wa kodi wanapewa wachache walaji wengi

Hii sio sawa why wasipewe dp world?

Takukuru pia
Napendekeza kadharika
Taasisi ya nida na rita
Wapewe wawekezaji ambao wataongeza ufanis
Upatikanaji wa namba vitambulisho
Kona nyingi sana

Tume ya uchaguzi sisi kwetu ni kazi sana
Na yapo maeneo mengi ambayo tumekwama kiutendaji
Tuwape wengine wajaribu

Ushajiuliza kuhusu ajira portal? Au utumishi wenyewe?
Kwann tubaki nao

Sgr tren ya mwendo kasi
Tumetumia pesa nyingi kutengeneza reli ila tuneshindwa kuleta au kununua behewa za kuendana na reli yetu kwa ubora
Behewa ni kawaida sana

Kwann tusiwape wawekezaji wakatusaidia eneo hilo?

Tanesco hata wakichukua dp world miaka 1000 sawa wenyewe mnaelewa kwann tumeendelea nayo sisi mpaka sasa?

Zanzibar ni sehemu yetu ya jamhuri swali kwsnn ikulu zote mbili zipo bara? Napendekez ikulu kuu iwe zanzibar
Hizi za bara ziwe ikuku ndogo
Pia zitasaidia sana kuimarisha muungano

Machache hayo lakini yako maeneo mengi
Tuyafanyie privatizations kwa wenye uwezo kama tulivyokuba kubaliana katika bandari

Kazi iendelee
Mama mpaka achoke mwenyewe sisi mpaka mwisho naye

Hakika kaupiga mwingi sana
Hakuna kama mama
 
Kwakuwa TRA imekuwa moja ya sehemu zenye ufanisi mdogo na utendaji mbovu kabisa serikalini, ni kwanii mamlaka hii isibinafsishwe hata kwa waarabu tu ili kuongeza tija na ufanisi katika ukusanyaji mapato

Ni kipi ninyi waafrica mtakuja mkiweze.

Kila kitu hatuwezi wala hatujifunzi ili tuweze.

Basi hata serikali ibinafsishwe tu maana hakuna tunachoweza.

Kuanzia rais mpaka balozi wa nyumba kumi wote watoke dubai

waje watuongoze, maana hakuna tunachojua sisi ni maquma tu
🤒🤒🤒
 
Huku halmashauri ,ushuru unakusanywa na kampuni binafsi then wanapeleka mapato serikalini.
Watanganyika hatulipi Kodi kwa wingi.
Naunga mkono hoja TRA apewe mwekezaji,tumuwekee tu lengo Kila mwezi atupe shilingi ngapi.
 
Kwa Ripoti za CAG za kila mwaka sinavyo onyeshwa pesa inavyo tumika vibaya bila wahusika kuchukuliwa hatua ni bora kabisa kubinafsisha Serikali Nzima.

Hata wakija hao DP. World na kuongeza mapato mala Elfu Bandarini, mapato hayo yataishia kuliwa tu huku wahusika wakitamba mitaani.

Leo kama kama Mkoloni wa Kiingereza asingefukuzwa Tanzania na kuendelea kutawala.
Tanzania ingelingana na nchi za Ulaya Kiuchumi.

Nchi za Waafrika Weusi haziwezi kupiga hatua shauri ya watendaji wake kufikiria namna ya kuiba pesa tu. Ubunifu ni 0%.
Ikiwemo Tanzania.
Leo tunashangilia kubinafsisha bandari. Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa tunatamani tubanafsishe kila kitu kwa watu wa Nje ya Nchi.

Kwakuwa sisi tumefeli kuendesha secta zote za uchumi.
Ina maana elimu yetu ni 0%
Wasomi wetu ni 0%
 
Siku mkisikia TRA inauzwa nisitueni mapema ni compete namie kuinunua.
Pia msisahau Bunge, Ikula na hata mahakama hivi navyo vinaweza kunifaa.
 
Back
Top Bottom