Wananchi hebu mnifahamishe ni kweli? Kama ni kweli nyinyi wananchi mnasemaje?
Sawa nimeelewa kwani aliniambia ada ya mtihani wa NECTA ni Tshs 50,000/= bila penalt na MOCK EXAMS ni Tshs 15,000/= jumla ni Tshs 75,000/=. Naona sasa hata elimu imekuwa anasa, poa tutakwenda hivi hivi mdogo mdogo. Nashukuru kwa maelezo yenu.mkuu kwa waraka na barua wanatakiwa kulipa 50,000/- tena kwa kipindi fulani baada ya hapo kuna penalt kama unataka maelezo ni pm namba yako nikupe
Za mchana wakuu.
Nilipigiwa simu na ndugu yangu alioko mbali na ninapoishi. Akaniambia kuwa anahitaji nimsaidie ada ya mtihani wa form four,nikamuliza ni shilingi ngapi? akaniambia Tshs 50,000/= Nikashangaa!! Nikajua anataka kunipiga changa la macho. Wananchi hebu mnifahamishe ni kweli? Kama ni kweli nyinyi wananchi mnasemaje? Binafsi kama ni kweli naona hayo maisha bora kwa kila mtannzania hayapo. Kwa walioko mjini hebu tujadili hili.
tuache utani, elimu yetu itaendelea kushuka kila mwaka. Kama ada ya mtihani wanapandisha kama pledge za harusi bila kutoa pubic notes sidhan kama kuna tupo serious na elim yetu. Au ndo imepanda sambamba na umeme na maji? Nawashauri wanafunzi wawakomoe NECTA kwa kufaulu kwa wingi tuone kama wataendelea kupandsha.
Unajua kilichonishangaza sikusikia hata tangazo redioni kuhusu huu upandaji wa ada ya NECTA, halafu ada ya shule kwa mwaka ni tshs 40,000/- na unalipa kidogo kidogo, lakini huku vijijini wazazi wanashindwa kulipa hiyo ada, sasa hii ya 50,000/= kwa mkupuo itakuwaje? na kwa muda mfupi hivi? Mimi nafikiri wanatakakuzuia matokeo ya wadogo zetu. NECTA ilitazame vizuri binafsi sioni kama ni sawa.tuache utani, elimu yetu itaendelea kushuka kila mwaka. Kama ada ya mtihani wanapandisha kama pledge za harusi bila kutoa pubic notes sidhan kama kuna tupo serious na elim yetu. Au ndo imepanda sambamba na umeme na maji? Nawashauri wanafunzi wawakomoe NECTA kwa kufaulu kwa wingi tuone kama wataendelea kupandsha.